Ads

STAA WA FILAMU NCHINI @ LULU AUKWAA UBALOZI WA LUMINA SKIN


STAA wa Filamu nchini Elizabeth Michael@Lulu ambaye ni balozi wa Lumina Skin amevutiwa kufanya kazi na luminaskintz kutoka na ubora wa bidhaa hiyo kwani jina lake linamaanisha mwangaza kwa Kila mtumiaji .


Hayo ameyabainisha Leo Agosti 13,2025 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari,Lulu amesema kwamba bidhaa hiyo Ina ubora  na viwango vya kimataifa kutokana na vitu mbalimbali ambavyo vimetumika katika  utengenezaji wa bidhaa hiyo.


Aidha ,amesema kwamba kwa mtu yoyote atakaye tumia bidhaa hiyo humuacha kama alivyo kwani haichubui ngozi hubaki katika ngozi yake ya asili


Kwa upande wake Meneja Masoko wa luminaskintz Osmunda Ndimbo amesema kwamba wameamua kufanya kazi na Elizabeth Michael kutokana na ushawishi wake katika jamii.

No comments