BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA GBT YAONYA WANAO KIUKA SHERIA
KAIMU MKURUGENZI wa Huduma wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania(GBT) Daniel Ole Sumayan amesema kwamba michezo ya kubahatisha sio ajira ila ni burudani kwa wanaocheza kwenye michezo hii hakuna ufundi wowote wa kucheza Bali ni bahati.
Hayo yamebainishwa Leo Agosti 12,2025 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa GBT wakati wa mkutano na wahariri na waandishi vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa hazina.
Mkurugenzi Sumayan amesema kwamba GBT ina jukumu la kutoa leseni,kusitisha,kurekebisha pamoja na kushauri juu ya utozaji na ukusanyaji wa kodi na tozo nyingine mbalimbali za michezo ya kubahatisha.
Aidha ,ameongeza kwamba jukumu lingine ni kufanya ukaguzi kwa waendeshaji wa michezo ya kubahatisha ili kuhakikisha utekelezaji wa Sheria pia kulinda jamii dhidi ya madhara yatokanayo na michezo ya kubahatisha kama uraibu ,udanganyifu na kuzuia ushiriki wa watoto pamoja na kutatua migogoro baina ya waendeshaji na wachezaji.
Hata hivyo amesema kwamba Hadi Juni 2025 GBT imesajili kampuni 62 ya michezo ya kubahatisha pamoja na kutoa leaeni ya bahati nasibu ya Taifa 8549.
Sanjari na hayo ,GBT imechangia uchumi wa Taifa kwa Kodi ya michezo iliongezeka kutoka sh.bilioni 131.99 kwa mwaka 2020/21 kufikia shs.bilioni 260.21 kwa mwaka 2024/25 kwa ongezeko la asilimia 97 .
Sambamba na hayo amesema kwamba hadi juni 2025 wametoa ajira 30,000 ikijumuisha ajira rasmi na zisizo rasmi
Pia ameeeleza kwamba jumla ya shilingi bilioni 66.7 zimeingizwa nchini kutoka kwa wawekezaji wapya katika kipindi Cha miaka miwili iliyopita.
Aliendelea kwa kusema kwamba katika kipindi Cha miaka mitano iliyopita jumla ya shilingi bilioni 44.6 zilitolewa na baadhi ya waendeshaji kuendeleza michezo ili kuboresha michezo mbalimbali pamoja na miundo mbinu.
Pamoja na hayo lakini pia zipo changamoto zinazokabili sekta hii hasa waendeshaji wasio na leseni hususani mashine za sioti maarufu Dubwi kitu ambacho husababisha upotevu wa mapato ya serikali pamoja na kuendesha biashara ya mashine kiholela na ushiriki wa watoto na kuharibu taswira ya sekta hii kwa ujumla.
Alibainisha kwamba katika kipindi Cha mwaka 2024/25,GBT ilifanikiwa kukamata mashine zipatazo 790 katika maeneo mbalimbali nchini hivyo mashine hizo zisinge dhibitiwa zingeweza kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na Kodi,ada na ushuru
Post a Comment