TUME HURU YA UCHAGUZI INEC IMESEMA ITAZINGATIA SHERIA NA MAADILI YA UCHAGUZI
TUME huru ya Taifa ya uchaguzi NEC imewataka waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo , na maofisa ununuzi kutenga sehemu ya muda wao kwa kusoma katiba ,Sheria na maelezo mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo.
Lengo la kusoma katiba , Sheria na maelezo mbalimbali yanayotolewa na Tume Ili yaweze kuwaogoza katika kusimamia vyema uchaguzi utakao kuwa huru na haki.
Balozi Omar Ramadhan Mapuri mjumbe wa Tume huru ya uchaguzi , aliyasema hayo wakati wa ufungnzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi hao wapatao 108 kutoka halmashauri za Bagamoyo ,mkuranga, Rufiji, Chalinze zamkoa wa Dar es salaam na Pwani.
Aidha Tume huru ya Taifa ya uchaguzi inawapatia Mmafunzo haya kama sehemu ya kuwaongezea maarifa na uzoefu kwenye kipindi chote cha uchaguzi mkuu kwa kuzingatia Sheria na kanuni za uchaguzi .
Hata hivyo Sheria na miongozo kwa wasimamizi wa uchaguzi unawataka wapiga kura kutoka kwenye maeneo ya kata na mikoa kushiriki zoezi la upigaji kura linapaswa kuwa la haki kwa raia wa Tanzania.
Ameipongeza kwa kusema Tume huru ya uchaguzi inasimamia pamoja na kuratibu uendeshaji wa chaguzi kwa mujibi wa Sheria Ili kurinda Democrasia kwa manufaa ya wananchi , vyama vya siasa na wagombea
Post a Comment