Ads

EFM YABUNI MBINU MPYA KUFIKA FURSA KWA VIJANA

Na Francis Peter, Dar es Salaam

Kituo cha Redio cha EFM imebuni mbinu mpya ya kuwafika kundi kubwa la vijana kuzifika fursa kwa kuleta "Kitaa Hub".



Hatua hiyo imekuja baada ya kutimiza miaka 10 tangua kuanzishwa kwa kituo cha redio cha EFM  ikiwa na lengo kufikia kundi kubwa la Vijana.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Francis Sizza maarufu kama Majizzo amesema kupitia EFM atatimiza maono yake ya kuwainua vijana kupitia kampeni ya Majizzo Jobs Campaign.

Aidha amesema jukwaa la Kitaa Hub litakuwa jukwaa mahususi lenye lengo la kuwapa vijana nafasi ya kujifunza, kukua na hata kushindana katika soko la ndani na kimataifa.

“ Lengo letu ni kufikia kundi kubwa la vijana kwenye field tofauti tofauti, naongelea vinyozi, fundi uashi, wapishi, wasusi, dada wa kazi, madereva, wasanii, waandishi wa nyimbo, DJS na graduates na wengine wengi Kwa kifupi ni uwanja wa kujidai onyesha uwezo wako” Amesema Majjizo.

Kwa upande wake mjumbe wa timu inayosimamia jukwaa hilo Dkt Albert Komba amesema kwamba jukwaa la Kitaa hubs litasaidia kuwajengea uwezo vijana wanaotafuta ajira na kuwaunganisha na waajiri Kwa urahisi zaidi.

Aidha amesema kwa sasa kiwango Cha ajira chini kipo chini hivyo serikali na taasisi binafsi hazina budi kushirikiana kutafuta mwarobaini wa tatizo Hilo nakisusisitiza kuwa kupitia Kitaa hubs intasiadia kupunguza tatizo la ajira Kwa vijana ambao Wana vipaji vya aina mbalimbali.

“Hili jukwaa la Kitaa hubs pamoja na Majizzo jobs Compaign itaweza kukutanisha vijana nchi nzima ili kuweza kuonyesha vipaji vyao,naamini kuanzishwa kwa jukwaa hili itasaidia vijana kutoa mawazo yao,bunifu zao na kuweza kufikia ndoto zao Kwa urahisi zaidi” amesema Dkt Komba.

Hata hivyo vijana waliojitokeza katika mkutano huo wamepongeza kuanzishwa kwa jukwaa la Kitaa hubs kwani litawasaidia kuwasimamia katika kupata kazi nzuri na zenye staha huku wakisisitiza kuwepo Kwa usalama wa taarifa zao kwenye mtandao huo wa website.


No comments