Ads

DANCE CLUB YAJA KAMPENI KUZIVUSHA SIMBA NA YANGA KLABU PIGWA AFRIKA.

Na Francisco Peter

Kuelekea michezo ya robo fainali ya michuano ya klabu pigwa barani Afrika (CAF) kwa timu za Yanga na Simba Bar  Maarufu jijini Dar es salaam ya Dance Club imekuja na kampeni Maalumu ya kuhamasisha mashabiki wa timu hizo kushiriki katika kuwapa sapati  ili zifuzu hatua ya nusu fainali.

Hayo yamesemwa na  Meneja wa matukio na Burudani wa Bar hiyo Bw. Jafar ambapo ametaja  lengo la kuja na kampeni hiyo iliyopewa jina la  'Dance Club Tuvushe' ni ili kutoa chachu kwa mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga kuhakikisha wanahamasika kusapoti timu zao.

Amesema kuwa katika kampeni hiyo wametoa kadi maalum kwa mashabiki wa timu hizo ambazo zitawawezesha kuangalia michezo ya hatua ya robo fainali ya katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika kupitia screen kubwa zitakazofungwa ndani ya Bar hiyo.

"Tumeanzisha kampeni hii ili kuhakikisha mashabiki wanahamasika tutatoa kadi ambazo zitauzwa kwa shilingi elfu kumi na tutatoa fursa kwao mashabiki kuja kuhakikisha timu zao zinafuzu kwenda hatua ya nusu fainali na yote watayaona hapa dance club"amesema meneja huyo.

Kwa upande wao mashabiki wa timu za Simba na Yanga wamepongeza hatua ya bar hiyo kuja na kampeni hiyo,  huku wakiwataka mashabiki wenzao kujitokeza kwa wingi kuangalia mechi baina ya timu zao na mahasimu wao.

"Sisi kama Simba SC tutahakikisha timu yetu inamkalisha Al Ahly kwa Mkapa, kwani pale hatokagi mtu na tuna historia ya kumfunga Al Ahly naamini tutafuzu kwenda nusu fainali" amesema  Albert Oscar.

Naye Shabiki wa Yanga Shaban amesema Mamelodi hawatatoka salama ndani ya dimba la Mkapa March 30, 2024 kwani watahakikisha wanawapiga nje ndani.

No comments