WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata na kuwashikilia watu wawili wanaodaiwa kula njama na kumuua mwanamke aliyejulikana kwa jina la Barke Pesa Rashid (30) mkazi wa Ilala Utete Jijini Dar es salaam.
Taarifa ya jeshi la polisi imeelza kuwa tukio hilo limetokea tarehe 1.1.2022 tabata segerea kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Maridadi ambako tarehe hiyo mtuhumiwa wa kwanza jinsia bounser miaka (34) mkazi wa Segerea Kalabash Pub alifanya mipango ya mapenzi na mwanamke aliyemuua baada ya kula njama na mtuhumiwa mwingine wa pili aliyekamatwa mwenye jinsia kiume ‘White’ miaka (33) mfanyabiashara ya Lori la kuzolea taka mkazi wa Tabata Segerea.
Chanzo cha maauaji hayo ni Mwanamke huyo kukabwa shingo mpaka kupoteza maisha akiwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni na inadaiwa na mtuhumiwa wa kwanza alikodiwa na mtuhumiwa wa pili White kwa malipo ya Sh 1,700,000, ili amtongoze na baadaye aende kumuua mwanamke huyo kwa madai kuwa mtuhumiwa wa pili alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini ilidaiwa na mtuhumiwa wa pili kuwa mwanamke huyo ana wanaume wengine.
Mtuhumiwa wa kwanza amekiri kupewa Shs 1,200,000 kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai Sh 500,000 kwa mtuhumiwa wa pili kwa mauaji ya mwanamke huyo.
Uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
Post a Comment