Ads

SIMBA YAENDELEA KUGAWA POINTI LIGI KUU,LEO NI ZAMU YA KAGERA

 


Mwamba wa habari

Timu ya Kagera Sugar  wanankurukumbi  leo wamefanikiwa  kuzima ndoto za ushindi  kwa  Bingwa  mtetezi  Simba Sports Club kwa kushinda 1-0 katika mchezo uliopigwa  katika  dimba la Kaitaba Mkoani Kagaera.

 Simba kwa  mara ya pili  sasa wameendelea kugawa pointi katika mechi ya za Ligi Kuu ya NBC ambapo  pia hivi karibuni kule Mbeya wali chapwa bao 1-0 na Mbeya City na baadaye kutoa sare na Kagera Sugar mchezo uliopigwa uwanja wa Manungungu mkoani  Morogoro.

Shujaa wa Kagera Sugar ni Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba Hamisi Kiiza ambaye mnamo dakika ya 71 aliwanyanyua mashabiki wa Kagera baada ya kufunga bao lililo dumu hadi mwisho wa mchezo.

Hata hiyo shujaa huyo Hamizi Kiiza dakika ya 90 alionyeshwa kadi ya pili ya njano na  nyekundu baada ya kuupiga mpira wakati mwamuzi kapuliza kipyenga.

Kwa matokeo hayo Simba wamebaki na Pointi 25 huku wakiwa wamecheza mechi 13 na kuzidi kuachwa kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya Mabingwa  wa kihistoria  Vinara Yanga wenye Pointi 35 wakiwa wamecheza mechi 13 huku kagera wakipanda hadi nafasi ya 9 wakiwa na point 16 na michezo 13.


No comments