Wandishi wa habari 6 na watu wengine wanane wafariki dunia katika ajali mbaya ya Gari.
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Wanahabari, Ndugu Jamaa na Marafiki kufuatia ajali iliyohusisha magari mawili leo asubuhi na kusababisha vifo 14 ikiwemo vya Waandishi sita wa Habari.
Mkuu wa Wilaya ya Busega Gabriel Zakaria amesema gari ya waandishi wa habari ilikuwa na waandishi saba waliokuwa kwenye msafara wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Mwanza wakielekea wilayani Ukerewe, watano kati yao wamepoteza maisha papo hapo huku abiria sita nao wakipoteza maisha papo hapo.
Ameongeza kuwa majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa, watatu wamefariki dunia na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 14
Post a Comment