TANESCO YANG'ARA TUZO ZA NBAA.
Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA.
Leonard Mkude katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju,
Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu
nchini uliofanyika katika eneo hilo.
CPA. Mkude amesema kuwa taarifa bora za fedha ni muhimu sana katika
maendeleo ya nchi kwa kuwa walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine hutegemea
taarifa hizo katika kufanya maamuzi.
CPA. Mkude ni mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji tuzo, amewapongeza washindi
wote kwa kupata tuzo baada ya kufanya vizuri kwa kutoa taarifa ya fedha kwa
ubora unaotakiwa.
Afisa Mkuu wa Fedha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Renata Ndege,
amesema kuwa ni mara ya tano wanashika nafasi ya kwanza kwa kutayarisha
mahesabu kwa kutumia kiwango cha kimataifa katika kundi la mashirika ya umma.
Bi. Ndege amesema kuwa kupata tuzo hiyo imetokana na TANESCO kufata
utaratibu wa viwango katika kutayarisha mahesabau ya fedha za watanzania kwa
salama.
“Tutahakikisha tunaendelea tufata vigezo vinavyotakiwa wakati
tunatayarisha mahesabu, huduma zitaendelea kuboreshwa ikiwemo umeme unakuwa wa
uhakika “ amesema Bi. Ndege.
Amefafanua kuwa hakuna njia ya mkato ili uweze kupata ushindi pamoja na
zawadi, kwani ni lazima ufate taratibu za mahesabu ili uweze kushinda katika
mashindano haya.
“Taasisi nyengine zinatakiwa kuwa na uongozi bora pamoja na kufata
utaratibu wa mahesabu ili waweze kufanya vizuri zaidi na kuapata tuzo” amesema
Bi. Ndege.
Bi. Ndege ameishukuru serikali kwa kufanya uwekezaji wa miundombinu ya
umeme ili kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kupatikana wakati wote.
Tuzo za NBAA zinalengo kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kimataifa, ambapo washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu hapa nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha Hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa.
Post a Comment