Ads

Halmashauri ya Jiji yakabidhi mikopo ya shilingi bilioni 2 kwa vikundi 97.

 

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekabidhi hundi ya shilingi Bilioni 2 kwa vikundi 97 vilivyopo Wilayani Ilala vya Wanawake ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Akisoma taarifa ya juu ya Maendeleo ya Mfuko wa kuendeleza Wanawake na Watu Wenye Ulemavu kupata asilimia kumi ya mapato ya ndani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jumanne Shauri amesema katika vikundi hivyo 97 vya Wanawake 46 vyenye thamani ya shilingi 980,000,000/= vikundi vya vijana 43 thamani ya shilingi 890,000,000/= na vya watu wenye Ulemavu vinane vyenye thamani ya shilinhi 157,000,000/=.

“Vikundi hivi 97ambavyo leo tumewapa mafedha haya walishaandaliwa na maafisa Maendeleo wangu wa Jamii na wamewapa mafunzo na fedha zimeshaanza kuingizwa katika akaunti za vikundi vyao asilimia kubwa ya vikundi hivyo vilivyokabidhiwa hundi vyenye mfumo wa viwanda vidovidogo vinavyozalisha tofali,vyakula,Nafaka,nguo,viatu,dawa ,sabuni za usafi na usindikaji nyama “amesema Shauri.

Shauri amesema kuwa viwanda hivyo vilivyopo Wilaya ya Ilala inaonyesha halmashauri ya jiji la Dar es salaam inatekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwawezesha wananchi mitaji mikubwa yenye kuleta tija katika kupunguza changamoto .

“Pamoja na miradi mikubwa ya vikundi 13 halmashauri itaendelea kuwawezesha miradi mingine midogo midogo na kuisimamia miradi hiyo kama mama Lishe,Baba Lishe,wafugaji kuku,Mbuzi,ng’ombe,wakaanga samaki,ushonaji,ufumaji,Batiki Tie Dye “amesema Shauri.

Aidha amesema maonyesho hayo ni sehemu ya ufatiliaji na tathimini ya maendeleo ya vikundi vyote vilivyopata mikopo vimewezeshwa na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau ikiwa ni katika kutekeleza sera ya TAIFA ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 kuelekea miaka 60 ya UHURU .

Mkurugenzi Jumanne Shauri amesema maonesho hayo yamelenga kukusanya makundi ya Wanawake ,Vijana na watu wenye Ulemavu kupata mbinu ya ujuzi ikiwemo utunzaji wa kumbukumbu za fedha za masoko ya bidhaa zao kutoka kwa Wataalam kupitia taasisi za fedha kuwawezesha makundi hayo kutambua na kufanya tathimini ya fedha za mikopo zilivyowasaidia katika miradi yao.

Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala ameipongeza halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kuwa ya kwanza katika kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali.

Makala amewapongeza Wabunge wa Wilaya ya Ilala Madiwani wa halmashauri ya jiji Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa utekelezaji wa Ilani na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kutoa mikopo ya serikali isiyo na riba kuwakwamua wananchi kiuchumi.

No comments