SERIKALI KUZALISHA MEGAWATI 200 UMEME UTAKANAO NA JOTO ARDHI IFIKAPO MWAKA 2025.
.........................
Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ipo katika
utekelezaji wa kuzalisha megawati 200 umeme utokanao na joto ardhi ifikapo mwaka
2025.
Akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji joto
ardhi Tanzania (TGDC) Bw. Kato Kabaka akitoa taarifa ya mafanikio ya
uendelezaji joto ardhi Tanzania katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa
Tanzania Bara.
Bw. Kabaka ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru ikiwemo kujenga
uwezo wa ndani tokea kuundwa kwa TGDC mwaka 2013 ambapo wataalamu waliopata
mafunzo wameongezeka kutoka 7 hadi 30 kwa ngazi ya diploma hadi shahada ya
uzamili, taaluma ya joto ardhi ambayo utolewa nje ya nchini.
Mafanikio mengine ni
upatikanaji wa vitendea kazi kwa ajili yakufanya tafiti kama MT(5),
TEM(1),Radon Counter (1) na CO2 Flux (1) ambavyo vimegharimu shilingi bilioni
1.5.
Kutekeleza miradi ya kipaumbele,
kuendelea kuandaa miradi mingine ya joto ardhi,kukamilisha kuchoronga visima
vifupi vya utafiti, kuendeleza miradi ya matumizi ya moja kwa moja ya joto
ardhi, kubuni na kuendeleza Teknolojia mpya, kujenga uwezo wa Taasisi za ndani
ya nchi, Kujenga uwezo wakuchoronga visima vya joto ardhi, kushiriki katika
ushindani wa fedha za uendelezaji wa joto ardhi na kufanya kazi za ushauri
elekezi ndani na nje ya nchi.
Kamishina Msaidizi wa
umeme kutoka Wizara ya Nishati Styden Rwebangila, amesema Tanzania ina uwezo
wakuzalisha zaidi ya megawat 15,000 za joto ardhi (MWe).
“Megawati hizo ni kwa
ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya joto ardhi, mchanganyiko wa joto, maji
moto na madini una matumizi mbalimbali mtambuka ya kiuchumi na kijamii”amesema.
Amesema kuwa matumizi hayo
ni uchakataji viwandani, kuongeza thamani ya mazao ya kilimo,mifugo,ufagaji wa
viumbe wa majini,misitu hususani kukausha mbao,kivutio na kichocheo cha utalii
na tiba kwa magonjwa mbalimbali.
Amebainisha kuwa kabla ya
ukoloni chemchemi za maji moto ziliendelezwa kwa ajili ya tiba, matumizi ya
mifugo (magadi) ibada na kuimarisha utawala mila na utamaduni mfano Mtagata-
Kagera, Ibadakuli -Shinyanga na Amboni Mkoani Tanga.
Post a Comment