FIDES INSURANCE AGENCY YATOA SOMO ELIMU YA BIMA.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fides Insurance Agency Bw. Sayi John Daud ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Bima nchini akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
...........
Kampuni ya Fides Insurance
Agency LTD ambao ni wauzaji wa
Bima mbali mbali iliyopo Tabata Segerea jijini Dar es Salaam imesema
wanananchi wakiwa na bidii ya kukuza uelewa juu ya bima zinazotelewa na makampuni italeta ahuweni
wakati wa majanga.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Fides
Insurance Agency Bw. Sayi John Daud, amesema kuwa wananchi wakiwa na uelewa itachochea kupunguza majanga.
"Kuna baadhi hawana uelewa na bima, hivyo jamii ikiwa na
uelewa zaidi itasaidia kuepukana na majanga mbali mbali zidi ya umiliki wa
vyombo vyao mbalimbali,"amesema Bw. Daudi.
Bw. Daudi ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Bima nchini,
ameeleza kuwa jamii inatakiwa kukata
bima kwa kumaanisha ili kuepukana na changamoto ikiwemo kulipwa pale nyumba yako
au gari na matatizo ikiwemo ajali.
Ameeleza kuwa tayari serikali ipo katika mpango wa
kuhakikisha inawafikia asilimia 80 ya watanzania kuwa na uwelewa wa bina pamoja
na asilimia 50 wawe wamepata bima hadi kufikia mwaka 2030 .
Daudi amesema kuwa
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini ( TIRA) imekuwa ikichagiza kufikia malengo ya serikali ambayo ni muhimu kwa
Mawakala , Madalali pamoja na makampuni ya Bima kuendelea kutoa elimu kwa
wateja.
Almefafanua kuwa wao
kama wakala wamekuwa wakijitaidi kila
mmoja awe na kitu cha kipekee ili wanaoshindana wasiweze kushindwa katika kutoa huduma.
Post a Comment