Ads

MGOMBEA UDIWANI KATA YA TUNGI,NIMEFANIKIWA KUTEKELEZA MENGI

 



Na John Luhende 

Mwamba wa Habari

Mgombea kiti Cha udiwani CCM kata ya Tungi Kigamboni Ndugu Ernest Mafimbo amewaomba wananchi wa kata ya Tungi kuchagua Chama cha Mapinduzi na  kumchagua ili awezekuwa kuwaletea Maendeleo.


Amesema hayo Katika mkutano wa kampeni uliofanyika  Katika eneo la mnadani Tungi akiambatana na Mgombea ubunge wa chama hicho Dkt Faustine Ndugulile ikiwa ni mwendelezo wa kampeni .

Amesema,akiwa madarakani  alifanikisha kujenga ofisi za serikali za kata hiyo kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi na Mbunge ,pia alifanikisha kujenga ofisi za Mitaa ya kata hiyo ambapo mwanzo walikuwa wakipanga .


Pia alifanikisha kujengwa vyoo  vyenye thamani ya shilingi milioni 38 Katika shule ya msingi Tungi na madarasa mawili yanayoendeleakujengwa .


Kwajuhudi zake pia amesema, alipata ufadhili wa kampuni ya mafuta ya  TAZAMA na kuanza kusambaza Maji kwa wananchi wa mtaa wa  magogoni ,na  alifanikisha kujengwa kwa barabara  kiwango cha changarawe  Katika eneo korofi la pale kwa masisita kuelekea soko maziwa  ambapo wakati wa mvua maji yalikuwa yanajaa.

" Wananchi naomba mjue kuto fautisha chama na vyama , CCM ndiyo chama ,,,vile vingine ni vyama vya watu Chagueni  CCM ,Mimi nilikuwa chama Cha upinzani nilikuwa  sawa na tochi iliyo ili wekwa gunzi badala ya betery haiwezi kutoa mwanga "Alisema .


Uwezo wa kufanya kazi utatokana na maamuzi ya wananchi kwa kuchagua  CCM ili kuweza kuyaendeleza mazuri ambayo imekwisha yaanzisha na kwa kata ya tungi itanufaika na mradi wa bara bara na mifereji unaotekelezwa na DMDP amabapo mwanzao  haikunufaika .

No comments