Ads

Watanzania watakiwa kujitokeza kuchangia Damu Moi

Kuelekea mpambano wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga siku ya Jumapili Julai 12 mwaka huu 2020, Mfanyabiashara Azim Dewj amewaomba watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kuanzia kesho.

Ombi hilo linalo gusa watanzania kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wahitaji wa damu ikiwemo,majeruhi wa ajali,wajawazito,na wengne wanaofanyiwa upasuaji

Hayo yamesemwa na Dewj leo jijinj Dar es salaam ambaye pia ni muhamasishaji kampeni ya uchangiaji damu salama kwa wanaopenda michezo ambapo alisema kampeni hiyo inaanza kesho saa tatu katika maegesho ya zamani ya taasisi ya Mifupa Hospital ya Mhimbili (MOI) .

"Kila atakayechangia atapatiwa zawadi ya jezi ya klabu ya Simba na Yanga yenye thamani ya shilingi 15000," alisema Dewj.
Alisema uchangiaji wa damu ni kitendo cha ubinadamu kwani hupendezwa ma Mwenyezi Mungu kuokoa maishaa ya watu ambao wengie huja hospitali wakiwa hali zao ni mbaya hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi jezi zilishatolewa kila klabu imetoa jezi 100 za kuanzia.
Dewj alisema zoezi hili ni endelevu jamii kutambua uchangiaji damu haitaoshia Dar es salaam itaenda hadi mikoani kwani wangonjwa wanaohitji damu wako kila hospitali hivyo jamii imeombwa ijitokeze kujitolea damu mara kwa mara.
"Uhitaji wa damu ni mkubwa zaidi kwani licha ya taasisi ya moi inayohusika na mifupa bado kuna wagonjwa wengine ikiwemo upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa nao wanatumia damu nyingi"alisema Dkt .Swai.
Kwa upande wake mkurugenzi wa tiba MOI Dkt. Samweli Swai amesema taasisi hiyo inamahitaji makubwa ya damu kwani kwa siku hutumia takribani unit 30 za damu hivyo kwa mwezi mzima huitaji uniti 1,000. Ameongeza kuwa tokea kuanza kwa ugonjwa wa COVID 19 ,uchangiaji wa damu kwa hiyari ulipungua hivyo zoezi hilo litakalofanyika kesho litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya damu.
Naye mwakilishi wa mdhamini wa Klab ya Yanga GSM ,Mhandisi Hersi Said alisema walipokea wazo hilo kutoka kwa Azim Dewij na Kama sehemu ya watanzania wameunga mkono na watendelea kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ili kupunguza changamoto zilizopo.

Kwa upande wake mwakilishi wa timu ya Simba kutoka Romario Sports 2010 Ltd Muna Jingu amesema jitihada za kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari zinatakiwa kuongeza hivyo ni wajibu taasisi na kampuni nyingine kujitokeza kuongeza motisha.

Katika kipindi kilicho pita Dewj aliweza kutia nguvu katika uchangiaji kwa kutoa ofa ya tiketi 300 kwa mashabiki (Yanga na Simba) ambao walijitokeza kuchangia damu MOI ili kuokoa maisha ya majeruhi

No comments