Ads

(ASF) Elisa Mugisha :Tumekuwa Tukitoa Elimu ya Kutosha kwa Umma Kuhusu Kujikinga na Majanga dhidi ya Moto.

(ASF) E.Mugisha  wa Jeshi la Uokoaji Ilala jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari jiji  Dar es Salaam hivi karibuni.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala limesema limekuwa likitoa elimu ya kutosha kwa umma kuhusu kujikinga na majanga dhidi ya moto.

Ambapo limetoa rai kwa wauza vifaa vya kuzimia moto wote watatakiwa kuwa na vibali kutoka Jeshi hilo na kuwa vibali hivyo vinapatikana kwa tozo ya shilingi 200,000.

 (ASF) Elisa Mugisha amesema kuwa awali tozo  hiyo ilikuwa ni shilingi 500,000 baada ya kufanya maboresho tozo hizo zimepunguzwa hadi shilingi 200,000.

Anasema katika elimu ya kinga mkoa wa Ilala ambapo katika shule mbali mbali zinazo wazunguka ambapo wanafunzi wamekuwa mabalozi wazuri katika kutoa Elimu ya Kinga na Tahadhari ya moto hata majumbani.

Katika hatua nyingine Mkoa huo umekuwa na karakana ambayo inatengeneza magari na mitambo yote ya Jeshi.

Hali katika changamoto zimekuwepo katika miundo mbinu ya barabara katika Mkoa huo ikichangiwa pia na foleni za magari.

Pia wananchi kushindwa kuweka vifaa vya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto ambavyo vingewawezesha kukabiliana na majanga ya moto pale yanapotokea kabla ya kupata msaada wa gari la zimamoto.

"Yanapotokea  matukio tunaomba wananchi  waweze kufanya huduma ya awali kabla hatujafika katika tukio sambamba na hilo tutaendelea kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto katika maeneo yote ya Mkoa wa Ilala," alisema (ASF) Mugisha.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala jijini  limesema limeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na miongozo ya Jeshi.

( ASF)Mugisha amesema dhima ya Jeshi hilo ni kuokoa maisha na mali ,kuelimisha kujikinga na majanga ya moto na maokozi.

Alisema mpango kazi wao mwaka 2020 ni kutoa elimu kwa umma dhidi ya Mahabharata ya moto pamoja na kuwatayari muda wowote.

"Mambo mengine ni kuokoa maisha na Mali,kufanya ukaguzi wa Kinga na Tahadhari ya moto katika maeneo yote ya Mkoa wa Ilala," alisema ASF Mugisha.

Amesema elimu kwa umma imetolewa kwa wananchi kupitia mikutano ya serikali za mitaa,mashuleni ,masokoni na biashara na pia wamefanikiwa kutoa elimu kwenye Televisheni na Radio kwa vipindi 122.

Alieleza kua hata hivyo elimu ya kinga na tahadhali ya moto imeendelea kutolewa kwenye sehemu mbali mbali za mikusanyiko kwa jumla ya maeneo 100 ya Mkoa wa Ilala.

Alibainisha kuwa katika kipindi cha 2010 na 2020 wamepokea miito 139 na miito ya maokozi 42 hivyo kufanya jumla ya miito 181 ya moto na maokozi.

Jeshi hilo limeeleza limechunguza matukio ya moto yaliyotokea katika kipindi cha mwaka 2019 na 2020 yalisababishwa na matumizi mabaya ya vifaa vya umeme zikiwa zimewashwa hata kama hazina matumizi.

ASF Mugisha alisema Mkoa wa Ilala unakitengo cha maokozi majini ambacho kinafanya kazi nchi nzima panapo hitajika maokozi.

"Mwaka huu maokozi makubwa yamefanyika katika kijiji cha Mturo Rufiji,Bagamoyo ,Njinjo,Lindi Mka wa Pwani ambapo kulikuwa na mafurikoyaliyo kuwayamezunguka makazi na maokozi mengine yalifanyika mto Wami," Alisema.

Amesema katika kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari  dhidi ya moto ulioambatana na tozo ambapo katika Mkoa wa Ilala walipangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni moja tayari wamefanikiwa kukagua maeneo 8500 jumla ya shilingi 1248875,000 na kufanikiwa kuvuka malengo kwa asilimia 24.8.

Kwa hatua hiyo Jeshi hilo limetoa shukrani za dhati kwa wananchi kwa ushirikiano na limeeleza juu ya mambo waliyoyapata katika ufadhili wa vifaa mbali mbali.

ASF Mugisha amesema wamepokea misaada mbali mbali mfano ; katika chumba cha vifaa vya upumuaji wamepokea misaada ifuatayo kutoka kwa wadhamini kama Back plate aina ya PSS 5000 -50 ,Back plate aina ya Drager-122.

Baadhi ya misaada mingine waliyopokea anasema kuwa ni Back late ambazo hazijatimia  aina ya Drager-25 ,Tester ya face mask-02 ,Euro tester -01,Filter za compressor-05,BA Cylinder aina ya Carbon-16 ,LDV-200,Pneumatic system-10 pamoja Face mask-07,Comressor-01.

No comments