WATU WAWILI WAKAMATWA WAKISAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROIN
a Maria Kaira,Mwambawahabari
amlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawashikiria watu wawili kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 508.163.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji amesema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Kibo Ubungo January 27 mwaka huu wakiwa na gari aina ya Sienta rangi ya Silva yenye namba za usajili T 776 DSE.
Hata hivyo watuhumiwa walikamatwa ni Sultan Ngowi mwenye umri (24) Mchaga mkazi wa Tabata segerea na Jimmy Mlaki miaka (24) Mchaga mkazi wa Kinondoni Dar es salaam ambapo walikamatwa na mzani pamoja na nyaraka mbalimbali wanatarajiwa kupelekwa mahakamani muda wowote.
Aidha Mmlaka inawakumbusha Vijana kutojihusisha na biashara haramu Wala matumizi ya dawa za Kulevya atakayeshiriki atachukuliwa hatua stahiki za kisheria ikiwemo kifungo Cha maisha

Post a Comment