Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Yatoa Angalizo la Mvua Kubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa leo Jumatatu Februari 3, 2020 kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa na Ruvuma.
Taarifa iliyotolewa na TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.


Post a Comment