WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUHUWISHA LESENI ZAO
Mwambawahabari
Na. Catherine Sungura-Kasulu
Wataalam wa kada mbalimbali za afya nchini wametakiwa kuhuwisha leseni zao kila mwaka.
Hayo
yamesemwa na msajili wa baraza la wafamasia kutoka wiza ya afya
Elizabeth Shekhalage wakati akiongea na watumishi wa hospitali ya
halmashauri ya mji kasulu kwenye ziara ya katibu mkuu wa wizara ya afya
Msajili
amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mabaraza ya kitaaluma,kila
anayestahili kuwa na leseni ni wajibu wake kuzingatia takwa hilo na
hivyo kutimiza kwa mustakabari wa taaluma zao
"Kila
mwaka mnatakiwa kutoka kwenye gazeti la serikali,hakikisheni wote mna
leseni ili mtimize takwa la kisheria".Alisisitiza Shekhalage.
Kwa
upande mwingine Shekhalage aliwataka watumishi wa afya wenye maduka ya
dawa,wawe na maduka ya mfano kwa kusajiliwa kwani hakuna kifungu
kinacho wazuia wasiwe nayo.
Aidha, aliwataka
watumishi hao kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi holela ya dawa
ambayo husababisha usugu wa vimelea vya dawa kwa binadamu.
“Matumizi
yasiyo sahihi ikiwemo kutumia dawa bila.kuzingatia maelekezo
yaliyotolewa na wataalam au kutotunza dawa vizuri husababisha athari
nyingi kwa binadamu ikiwemo kuongezeka kwa ugonjwa ama madhara yasiyo ya
lazima kwa wagonjwa".Alisisitiza
Hata hivyo
aliwataka wananchi kuacha kununua dawa bila kwenda kwenye kituo cha
kutolea huduma za afya kupara vipimo na kupata ushauri kutoka kwa
wataalam.
a
Post a Comment