Ads

WAJASILIAMALI WATAKIWA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MILIPUKO

Mwambawahabari

Na.Catherine Sungura-Chato

Wajasiliamali wote nchini wametakiwa kujikinga dhidi ya magonjwa ya milipuko wanapofanya biashara zao ndani na nje ya nchi

Elimu hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula wilayani hapa kwenye kongamano la wajasiriamali lililoandaliwa na Chama cha Wanataaluma Waadventista Tanzania (ATAPE).

Amesema kongamano hilo la wajasiriamali, ni tendo jema lenye baraka, "nimekuwa kwenye ziara mikoa ya kigoma na kagera  tukiangalia utayari wa nchi hususan mipakani, namna tulivyojiandaa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama ebola na Corona".

Dkt. Chaula amesema kongamano hilo limewakutanisha wajasiriamali wengi, wajasiriamali wapo nchi nzima, mikoa halmashauri kata vitongoji hadi vijijini kwahiyo ni fursa nzuri ya kupatiwa elimu juu ya dalili pamoja na jinsi ya kujikinga na magonjwa ya milipuko kwakuwa  wao wanakutana na watu wengi na wanasafiri mara kwa mara.

"Nimefika Chato usiku  nikaelezwa kuhusu uwepo wa kongamano hili, nikasema sitaondoka bila kufika hapa nizingumze nanyi, maana magonjwa ya milipuko yameripotiwa kwenye maeneo mbalimbali hasa Ebola na Corona, nchini mwetu hatuna magonjwa haya.

"Lakini hatutaki kunyanyapaana, tunapaswa kuelimishana jinsi ya kuzuia na kujikinga tusipate,Hivyo, mnapokutana mnapata mawazo mbalimbali, kwa mfano kwenye kilimo tutalimaje, tutapandaje na tutavunaje na kupata soko la uhakika, Tanzania tuna rutuba, maji ya kutosha hatupaswi kuwa na njaa wala maradhi.

"Aidha,Dkt. Chaula alisema amefarijika kuelezwa kwamba kwenye kongamano hilo  watapata huduma ya kiroho (neno la Mungu) na kimwili (uchunguzi wa afya na matibabu), ni sehemu nzuri kupata elimu namna ya kujikinga na maradhi mbalimbali na jinsi ya kupata tiba.

Hata hivyo aliwasisitiza wajasiriamali hao kukata bima ya afya "Gharama za matibabu zimekuwa ghali, kongamano hili mmepata wadau wamewawezesha lakini ili jambo hili liwe endelevu, ni muhimu kila mwananchi akate bima ya afya ili aweze kupata huduma popote pale aendapo baada ya kumaliza kongamano hili," alisisitiza.

Alisema kukata bima ya afya ni jambo la hiyari lakini la lazima kwani hakuna anayejua kesho itakuwaje.

Akizungumza, mratibu wa Kongamano hilo, Dkt. Samwel Kikaro alisema wanatarajia kuona na kutibu watu 3,000 ndani ya siku saba kuanzia jana.

No comments