MEYA ILALA AONYA WENYE VITI SERIKALI ZA MITAA KUTUMIA VIBAYA NYADHIFA ZAO.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akihutubia wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Ilala (hawapo pichani) katika uzifunguzi wa semina elekezi iliyo fanyika katika ukumbi wa Tambaza Sekondari (Picha na Mwamba wa habari)
Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Ilala wakifuatilia kwa makini hotuba ya Meya .
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jumanne Kiangio Shauri akizungumza na wenyeviti wa mitaa hawapo pichani .
Na John Luhende
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amewataka wenyeviti wa Serikali za mitaa Wilayani Ilala kutumia vizuri nyadhifa zao vizuri kwa kujiepusha na vitendo vya rushwa ikiwemo kuwaonea wananchi kwa kuuza ardhi na kuchochea migogoro.
Kumbilamoto ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti hao iliyoandaliwa na manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais tawala mikoa na serikali za mitaa kwa lengo la kuwa jengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao na kuwataka kuiona kazi hiyo kama utumishi na wala siyo ajira bali waendelee na kazi zao.
''Uwenyekiti siyo ajira hizi ni kazi za utumishi ,ombi langu kwenu endeleeni na kazi zenu msiuze viwanja vya watu msiji husijihusishe na vitendo vya Rushwa mtakakuja kufungwa"Alisema
Aidha amewaisistiza wenyeviti hao kuhusu kusimamia suala la ulinzi na usalama na kuzingatia sheria,na kuimarisha usalama ili kuvutia wawekezaji na kuacha kutumia ubabe kuwaonea wananchi .
Pamoja na hayo Kumbilamoto amempongeza Kurugenzi wa Manispaa hiyo Jumanne Shauri kwa kununua magari mawili ya kuzoa taka na kuwataka wenyeviti hao kwenda kusimamia vyema usafi katika mitaayao.
Kwa uande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jumanne Kiangio Shauri ame amewataka wenyeviti hao kuwahudumia wanachi kwa upendo.
"Mambo ambayo mnapaswa kumalizwa mtaani kwenu wananchi wanakuja Manispaa hii inamaanisha hamuwahudumii vizuri ,naomba mkafanye kazi sitaki kuona wananchi wanajaa ofisini kwangu"Alisema
Naye Ktibu tawala msaidizi Serikali mkoa wa Dar es salaam ,Mary Assey , amewataka wenyeviti hao kushirikisha wananchi katika maendeleo na kuzingatia sheria na kusimamia utekelezaji wa Ilani, na kuhakikisha kuwa wanaitisha vikao ama mikutano na kuwaeleza wananchi maendeleo na kutatua kero zao .
Nao baadhi ya wenyeviti waliopata fursa ya kuzungumza wameomba kuruhusiwa kukaa na mihuri badala ya jukumu hilo kuapewa mtendaji jambo ambalo wamesema linakwamisha utekelezaji wa majuku yao katika kuwahudumia wananchi.
Post a Comment