Ads

VIJANA WATAKIWA KUJIUNGA NA MAFUZO YA UFUNDI STADI VETA



Mmoja wa Vijana waliosoma chuo cha VETA akionesha bidhaa  alizotengeza  ,maonesho ya 4 ya bidhaa za viwanda vya Tanzania katika viwanja vya maonesho  sabasaba jijin Dar es salaam.

Na John Luhende
Mafunzo ya ufundi yanayotolewa na vyuo vya  ufundi VETA yamesaidia vijana wengi katika kujiajiri na kupunguza wimbi la vijana mtaani kukaa bila kuwa na shughuli maalumu.

Hayo yamebainishwa na Afisa uhusiano wa VETA , Dora Tesha , alipokuwa katika maonesho ya 4 ya bidhaa za viwanda vya Tanzania ,ambpo alitumia fursa hiyo kutoa hamasa kwa vijana kujiunga katika mafunzo ya ufundi stadi ili waweze kuendeleza utaalamu wao .

"Tuna mafunzo aina nyingi  yanayojulikana kama mafunzo yanayotolewa kwa mfumo wa  Uanagenzi....kijana anasoma akiwa chuoni na kiwandani "Alisema

Alisema faida nyingine ya mafunzo haya yanamfanya mhitimu kumaliza masomo huku akiwa na ajira tayari hata kama hata pata hapo ajira anakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ajira kwani ana kuwa anauelewa mkubwa .

Aidha alisema Serikali inagharamia kwa kiasi kikubwa mafunzo ya Ufundi  na mzazi anakuwa anachangia kidogo tu hivyo hakuna sababubu ya vijana kukaa wakizagaa mtaani bila kuwa na cha kufanya .

Pia aliweka wazi kuwa VETA kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri mkuu wamekuwa wakiwatambua vijana au mafundi wanaojifunza kupitia sekta binafsi kupita mfumo usiorasmi wanakuwa  wanafanyiwa tathmini ya ujuzi walionao na kupewa mafunzo kuziba mapungufu na wakufanya vizuri hutunukiwa vyeti.


"Katika maonesho haya tumekuja na vijana waliofanya kazi nzuri ya ufundi ikiwemo kubuni baadhi ya teknolojia tumewaleta hapa ili kuwakutanisha na wadu mbalilmbali "Alisema

Mwisho ametoa wito wazi na walezi kuwapeleka vijana wao katika   katika vyuo vya VETA ili kuwajengea  na kuwataka kutohofia gharama .

No comments