Ads

UDASA Wakutana kujadili miaka 58 Ya Uhuru.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) imetakiwa kutekeleza majukumu yao kwa vitendo katika kuhakikisha wanafundisha wanafunzi kwa ajili kuwajenga ili wawe na uwezo na ufanisi mkubwa katika kutekeleza majukumu kwa vitendo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mdahalo wa kumbukizi ya miaka 58 ya Uhuru Mwanataaluma Mzee Joseph Butika, amesema kuwa tanzania kuna wanataaluma wengi lakini katika utekelezaji majukumu ya kimaendeleo bado changamoto.

Mzee Butika amesema kuwa jambo la muhimu katika utekelezaji tunatakiwa kujenda tabia katika kufanya kazi ya ufanisi kitu ambacho kitaleta maendeleo kwa taifa.

"Sasa kuna wanataaluma wengi ambao tabia zao walagai, wapenda rushwa, hawatosheki...tunafundisha watoto wetu elimu ya namna gani" amesema Mzee Butika.

No comments