Ads

Rais Mstaafu Dkt. Mwinyi awapa somo wahitimu Chuo Kikukuu cha Kampala

Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Kampala- Tanzania (KIUT) wakiwa katika Mahafali ya Pili ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kimataifa cha Kampala-Tanzania (KIUT) Mhe. Rais Mstaafu Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi amewataka waitimu wa chuo hicho kuwa waaminifu na waadilifu kwa kutokushiriki katika matendo ya kifisadi ili kuunga jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli kati na kuleta maendeleo ya Taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Dkt. Mwinyi, amesema kuwa maendeleo katika uchumi wa nchi yeyote ile inategemea kuwekeza katika maarifa na ujuzi. 

Amesema kuwa matumaini yake kuona wahitimu wanapata kufaulu maarifa na ujuzi katika fani walizosomea kutokana jamii inatarajia wana upeo wa hali ya juu katika kupambana na changamoto zinazokwamisha maendeleo ya Tanzania.

"Tunawatunuku vyeti, stashahada na shahada mbali mbali, lakini uthibitisho mkubwa wa maarifa na ujuzi wenu utatokana na utendaji wenu huko muendako" amesema Dkt. Mwinyi.

Amesema kuwa katika utendaji wao wakumbukeni kuwa binadamu wote ni sawa, hivyo wasitoe huduma kwa ubaguzi.

Hata hivyo Dkt. Mwinyi amewataka wahitimu hao kujiendeleza katika masomo ya juu zaidi.

"Ningependa kuwahimiza mtilie maanani uaminifu kazini, nawasihi mkaiwakilishe vizuri Jumuiya ya Chuo Kikuu cha KIUT kwa kuwa waaminifu na waadilifu na kutokushiriki kwa namna yoyote ile katika matendo yoyote ya kifisadi" amesema Dkt. Mwinyi.

Baadhi ya wahitimu wa Chuo kikuu cha Kimataifa Kampala- Tanzania (KIUT)  wakiwa katika mahafali ya pili ya chuo hicho.
Dkt. Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo cha KIUT, ameupongeza uongozi wa juu wa chuo hicho pamoja na viongozi wengine  walioteuliwa katika ngazi za Vitivo, Idara na Kurugenzi kwa mafanikio yanayopatikana hivi sasa. 

Ameeleza kuwa kazi wanayoifanya kwa kushirikiana na jumuiya zote za chuo chetu ni nzuri na inaonekana dhahiri.

 "Kwa timu hii na utendaji huu, sitegemei turudi kwenye changamoto ambazo kmbukeni daima kwamba mmepewa dhamana kuongoza chuo hiki na ni imani yangu kwamba mtatimiza wajibu wenu ipasavyo ili kurudisha imani" amesema Dkt. Mwinyi.

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kimataifa cha Kampala-Tanzania (KIUT) Mhe. Rais Mstaafu Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi (kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Jamidu Katima wakiwa katika maandamano ya kuingia katika ukumbi kwa ajili hafla ya mahafali ya pili ya chuo cha KIUT.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Bw. Alhaji Hassani Basajjabalaba, amesema kuwa changamoto kubwa waliyokabiliana nayo katika miaka mitatu iliyopita ni chuo chetu kufungiwa na TCU kudahili wanafunzi kutokana na mapungufu mbalimbali.

Amesema kuwa kwa jitihada zilizofanyika, hatimaye chuo chetu kimeruhusiwa kudahili wanafunzi kuanzia Mwaka wa Masomo 2019 / 2020.

Bodi ya Wadhamini inawapongeza wafanyakazi na jumuiya yote ya Chuo kwa kazi nzuri iliyowezesha kuruhusiwa kudahili wanafunzi wapya.

Bodi ya wadhamini inafarijika zaidi kwa ushirikiano uliopo baina ya jumuia zote kuu za Chuo chetu chini ya uongozi na usimamizi.
Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Jamidu Katima, amesema kuwa amewapongeza wahitimu wote katika fani mbalimbali.

 Amesema kuwa wahitimu watakaotunuku ngazi ya elimu ya Astashahada, Stashahada na Shahada mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala – Tanzania.

Profesa Katima amesema kuwa kuna jumla ya idadi ya wahitimu ni 1148 kati ya hao kuna wanaume 624 na wanawake 524.

Amesema wahitimu 387 (wanaume 230 na wanawake 157) watatunukiwa Astashahada na Stashahada.

Wahitimu 761 (wanaume 394 na wanawake 367) watatunukiwa Shahada ya Kwanza

Wanafunzi watano (5) wamepata ufaulu wa Daraja la Kwanza na watapatiwa zawadi mbalimbali katika jitiada za kuwapongeza.

"Nawatakia mafanikio mema katika shughuli zenu mtakazoenda kuzifanyaza kujenga Taifa, kati yenu kuna wale ambao tumeishi nanyi kwa miaka 3, 4 au 5, na labda wengine zaidi ya hapo kutokana na sababu mbalimbali" amesema Profesa Katima.

Hata hivyo ameeleza kuwa wamewafundisha ili waweze kuyatawala mazingira kwa kuwa wabunifu katika utendaji wao.

Profesa Katima amawasisitiza wahitimu wakafanye kazi za kujitolea ili wapate uzoefu, huku akiwataka wasichague kazi za kufanya wala eneo la kufanyia kazi.

Msomi huyo amewataka wahitimu kuwa mabalozi wazuri wa Chuo hiki, popote pale watakapokuwa.

Kwa upande wa wahitimu wameonekana kuwa na furaha baada ya kumaliza masomo yao huku wakiwa na shauku ya kwenda kufanya vizuri katika jamii kupitia elimu yao.

No comments