Ads

NAIBU MEYA AFUNGUKA CHANZO VITAMBI NA MAKALIO MAKUBWA




Na John Luhende
Mwamba wa habari
Watanzania wametakiwa kubadili tabia za ulaji chakula kwa kuzingatia vyakula vyenye virutubisho na kuwa na utaratibu maalumu katika muda wakula .

Hayo yamebainishwa na Naibu Meya wa Jiji la Dar es salaam Abdala Mtinika katika semina ya Lishe iliyoandaliwa na shirikala GAIN kwa kushirikiana na ofisi ya katibu tawala na mganga mkuu mkoa kwaajili ya Madiwani wa Jijiji la Dar es slaaam ambapo alisema katika mkoa huo takwimu zinaonesha katika kila Watoto 10 kuna watoto wawili wanautapiamlo.

''Ulaji unakiwango ila watu wengi wanzidisha kiwango na hili limekuwa ni tatizo ndiyo maana unaona watu wanavitabi na wanawake wengine unaona wana makalio makubwa hayo ni matokeo ya kuzidisha chakula ni vema tubadilisasa utaratibu wa kula "Alisema.

Kwa upande wake Diwani wa kijijichi Eliasa Mtarawanje aliwataka wazazi hasa akinamama wajawazito kuzingatia mpangilio wa vyakula pia kwa Watoto chakula bora katika kipindi cha siku 100,000 za mwanzo ili kujenga afya akili zao.

"Tumepata semina hii tunataka sasa kwenda kufikisha ujumbe huu kwa wananchi wetu ili wakayazingatie na kuyafanyie kazi haya hatimaye tuwe na jamii yenye afya bora yenye afya "Alisema

Naye Diwani wa Mwananyamala Songoro Mnyonge aliwataka wananchi kuepuka vya kula vilivyo sindikwa yaani vilivyo pita viwandani mfano nyama kwa kuwa zinachangia saratani .

"Ukienda leo katika hospital mbalimbali utakuta Watoto wadogo wanaugua kisukari ,saratani kwa sababu ya kutozingatia ulaji chakula "Alisema

Pamoja na hayo Mnyonge ameshauri suala la Lishe lipelekwe mashuleni kuelimisha wanafunzi pia suala hili likuchuliwe na viongozi kwa ngazi ya kisiasa kama ilivyo kwa ugonjwa wa UKIMWI ambapo vingozi wanahamasisha wananchi namna ya kujilinda.

No comments