Ads

WATANZANIA WAMETAKIWA KUCHUNGUZA AFYA MARA KWA MARA.

Na Maria Kaira,Mwambawahabari.
Daktari Bingwa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo Muhimbili(MNH)Patience Njenje ametoa wito kwa watanzania  kuweka utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua magonjwa yanayoweza kusababisha kiharusi na kuyadhibiti mapema kwa kunywa dawa na kubadilisha mfumo wa maisha

Akizungumza na waandishi wa  habari leo kuhusu siku ya kiharusi ambayo huadhimishwa duniani Oktoba 29 kila mwaka. 

"Kwa siku Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inapokea wagonjwa wa kiharusi kati ya 3 hadi 4 kwa siku ambapo wengi wao wanafika kati ya siku 3 hadi 7 baada ya kupata kiharusi"amesema

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa kiharusi ni wa pili na kwamba unasababisha vifo kwa asilimia 11.8 baada ya magonjwa ya moyo. 

Dkt. Njenje amesema kiharusi ni ugonjwa wa tatu  unaosababisha ulemavu kwa watu kwa asilimia 4.5 duniani na hivyo kusababisha watu washindwe kufanya shughuli za kila siku kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya  kiharusi.

Akizungumzia tatizo la kiharusi, Dkt. Njenje amesema kuwa Kiharusi kinawapata zaidi watu wenye umri zaidi ya miaka 65, ingawa kwa sasa inaonekana pia tatizo hili linawapata watu wengi wenye miaka 45 au chini ya miaka 45, hivyo tatizo hili hivi sasa siyo la watu wenye umri mkubwa pekee yake.

Naye Dkt wa Mishipa Fahamu Ubongo na Uti wa Mgongo Mohamed Mnacho amesema kutokana na kuongezeka kwa tatizo la kiharusi nchini Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha kitengo maalumu ili kuwachunguza na kuwapatia tiba stahiki wagonjwa wanaopata tatizo la kiharusi nchini.

"zaidi ya asilimia 90 ugonjwa wa kiharusi husababishwa na shinikizo la damu. Lakini pia, magonjwa ya moyo, selimundu pia huchangia mtu kupata kiharusi"amesema

Dkt. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo kwa watoto, Dkt. Zameer Fakih amesema kuwa takwimu za dunia zinaonyesha kuwa mtoto mmoja kati ya watoto 4,000 wanaozaliwa kila siku hupata kiharusi na sababu kubwa ya kupata kiharusi kwa watoto ni magonjwa ya moyo na selimundu.

No comments