Ads

CCM shina la Pamba Road Wajipanga kwa uchaguzi.serikali za mtaa


VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Shina la Pamba Road  Jijini Dar es Salaam  wamewahimiza wanachama wa shina hilo kuwa tayari kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa .

Mwakah 2019 kuna uchaguzi wa serikali wa mtaa ambao mara nyingi hutoa picha ya uchaguzi mkuu ambao hufanyika mwaka mmoja baada ya uchaguzi huu wa Serikali ya mtaa.

Akizungumza na wanachama wa shina  hilo la  CCM  Mwenyekiti wa shina hilo Sophia Ngwile  alisema hupo  uhakika wa kushinda kwa asilimia 95 uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, akitamba kuwa katika Uchaguzi Mkuu mwakani, imejipanga kuongoza kwa kupata kura nyingi na bidii za kufanya hivyo zinaanzia katika mashina.

Alisema kwenye uchaguzi huo, Watanzania wenye sifa ya kupiga kura watawachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa watakaowaongoza kwa muda wa miaka mitano ijayo hadi mwaka 2024 ambapo yeye kama kiongozi anapenda kuona shina lipo katika hali kubwa ya kupiga kura na kuhakikisha ushindi unapatikana kwa wingi kupitia CCM.

“Naomba waliona sifa za kupata mikopo kuchangamkia mikopo  na wafike kwake kwa ajili ya kuwatambua  na si kwa mtu ambaye siye mwanachama wa shina,”alisema Sophia.

Aliongeza kuwa lazima kila kijana wanawake na wanaume kuhikikisha wanakadi za CCM katika shina hilo ili kuwa na wanachama hai kwenye chama hicho.
Naye Saleh Chitwanga ambaye ni katibu wa Chama hicho kupitia mkutano huo wa shina la Pamba Road alisema kuwa katika vuguvugu hilo la kuelekea uchagzi  huo lazima wanachama wawe la lengo moja la kuhakikisha ushindi unapatikana kwa asiliamia kubwa.

No comments