ZAHANATI YA MNYAMANI KUPATA NEEMA KUMBILAMOTO AWASHUKURU WADAU.
Mwambawahabari
Msitahiki meya wa ilala Omary Kumbilamoto amewataka makampuni kuiga mfano wa Jamii ya khoja shia kwa jinsi inavyojitoa kuunga mkono jitihada za serikali.
Kumbilamoto amesema jamii hiyo imeahidi kutoa msaada wa vifaa tiba kwa mradi wa kimkakati kwenye zahanati ya mnyamani buguruni zahanati ambayo Rais John magufuli alitoa milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ambayo tayari yamekamilika.
Amesema jamii ya Khoja shia imekuwa ikijihusisha kusaidia idara ya afya kwa manispaa ya Ilala kwenye humuda za macho na kwamba wametambua na kuunga mkono serikali katika k miradi ya maendeleo inayotekelezwa.huku mstahiki meya akiwakabidhi vyeti kama shukrani kwa kuthamini mchango wao.akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupima mtoto wa jicho.
Kwa upande wake mratibu wa kambi ya macho ALIRAJA BANDALI kutoka jamii hiyo ya Khoja shia amesema lengo lao ni kuona wananchi wanakuwa katika afya njema Ili kujenga Taifa Imara huku wakijipanga kutembelea zahanati ya mnyamani siku ya ijumaa.
Post a Comment