Ads

HALMASHAURI YA KINONDONI YAWAPA MWEZI MMOJA WAFANYABIASHARA WA COCO


NA HERI SHABAN
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni yawapa  muda wa mwezi mmoja na nusu wafanyabiashara wa Coco Beach kupisha eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa ufukwe wa  kisasa.

Tamko hilo limetolewa na Meya wa Manispaa ya  Kinondoni Benjamini Sita leo wakati wa kuzungumza na Wafanyabiashara wa Mihogo  katika ufukwe huo.

"Katika maendeleo lazima changamoto ziwepo vumilieni wakati wa mpito huu mara baada ufukwe wa kisasa kukamilika mtarudi eneo lenu baada kukamika ujenzi Mkandarasi atajenga kwa muda wa miezi sita "alisema Sita.


Meya Sita alisema Ofisa Masoko wa Manispaa na Mtendaji wa Kata hiyo wataenda kuwaorodhesha na kujua idadi yao wafanyabiashara wote wanaotegemea eneo la ufukwe huo kufanya biashara zao ujenzi ukikamilika waliokuwepo wote watapewa kipaumbele.

Alisema dhumuni la kikao hicho na wafanyabiashara ilikuwa majadiliano ya kuwafamisha eneo wanalohamishwa kwa muda  kwani kubaki eneo hilo wakati ujenzi unaendelea kwa usalama ni hatari lolote linaweza kutokea .

Alisema ufukwe huo wa Coco beach ujenzi wake umeanza jana rasmi na mkandarasi wa Kampuni ya Tanzania Bulding Works anajenga ufukwe wa kisasa kwa shilingi bilioni 13.6 fedha kutoka serikali kuu zilizotolewa na Rais katika miradi Mkakati .


Alimpongeza Rais John Magufuli na kumwaidi awezi kumwangusha katika utekelezaji wa miradi hiyo katika kuunga mkono juhudi zake na kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda .

Awali mmoja wa wafanyabiashara Asha Machupa alisema yeye ni Mjane anategemea kufanya biashara eneo hilo pesa anayopata anasomesha watoto   wake wapo chuo.

Aidha Asha alisema watakapoondoka eneo hilo atakosa pia pesa ya marejesho ya mikopo ya halmashauri ya Manispaa hiyo ambayo inatolewa kwa makudi ya Wanawake ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Mwisho

No comments