MCHUNGAJI KANISA LA KRISTO AIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI.
Kanisa la Kristo imeitaka kwa serikali kuwaondoa
watu waliovamia eneo wazi lililopo karibu na kanisa hilo maeneo ya Mwembe
yanga, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Wavamizi hao wameonekana wakileta usumbufu, wakati
waumini wa kanisa hilo wakiwa katika ibada, kwani wamekuwa na kelele
zinazotokana na wavamizi hao wakiwa katika majukumu yao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, Mchangaji wa Kanisa la Kristo Temeke Bw. Morris Chiuyo, amesema kuwa wavamizi
hao wamejenga banda katika eneo la wazi yenye namba 307/A pamoja na kuwepo kwa
watu wanaofanya kazi ya kutengeneza magari kinyume na sheria.
Mchungaji Chiuyo, amesema kuwa katika eneo hilo wazi
kuna Gereji, Mama ntilie, Muosha magari, Dalali wa kuuza magari pamoja na soko
la ndizi.
“Watu wa gereji wanajisaidia kwenye ukuta wa kanisa
na wanamwaga girisi na oil na matambala machafu kitu ambacho sio rafiki”
amesema Mchungaji Chiuyo.
Ameeleza kuwa kanisani bado linayo imani kwa viongozi
wa serikali katika kusimamia sheria ili haki iweze kutendeka kwa namna moja au
nyengine.
Amefafanua kuwa wametoa taarifa katika mamlaka
mbalimbali lakini mpaka sasa hakuna hatua ilichukuliwa.
“Viongozi wenye dhamana ya kusimamia watanzania
kwenye maeneo ya haki wanapaswa kufanya hivyo ili kuleta maendeleo”
Kanisa la kristo Temeke lipo nchini mpaka sasa ni miaka 60 likifanya kazi ya kitume kwenye kiwanja namba 21,22 na 23.
Post a Comment