Ads

KINONDONI YAFUNGA UFUKWE WA COCO BEACH




NA HERI SHAABAN
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni leo imefunga ufukwe wa Coco Beach kwa ajili ya kujenga ufukwe wa kisasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo Meya Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sita alisema ujenzi wa fukwe huo unajengwa na Mkandarasi wa Kampuni Tanzania Bulding Works ltd.

"Ufukwe wa Coco beach leo unafungwa kwa muda wa miezi sita kwa ajili ya kujenga mradi Mkakati wa serikali fedha kutoka serikali kuu  Hazina "alisema Sita.

Meya Sita alisema gharama za Mradi huo shilingi bilioni,13.6 mradi wa fukwe huo ni mradi wa awamu ya pili mradi mwingine ni soko la Tandale   ambao nayo imejengwa na fedha za serikali mkataba yake ilisainiwa February mwaka huu.

Alisema ujenzi huo utajengwa kwa wakati ili wananchi waweze kutumia amewataka watoe ushirikiano.

"Namuakikishia Rais wangu John Magufuli nitasimamia mradi huu vizuri  pamoja na miradi mingine iliyopo katika wilaya yangu siwezi kumwangusha itakwisha kwa wakati" alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumjuli alisema wakati ujenzi unaendelea wafanyabiashara wengine ambao wapo eneo hilo watahama taratibu .

Aron alisema Mkandarasi walimpa tenda hiyo Tanzania Bulding Works ltd ni mzawa wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo  ajakabidhiwa fedha lakini tayari ameanza ujenzi.

Alisema eneo hilo wanajenga Resturant,uwanja wa michezo wa kisasa na huduma zingine .

Awali Meya wa Kinondoni wakati akizungumza na wandishi wa habari alisema mara baada mradi huo wa  ufukwe kukamilika wananchi wataingia bure bila tozo


Mwisho
Kinondoni
Septemba 17/2019

No comments