Ads

VIJANA WA JAMII MPYA YA RAIS MAGUFULI WAUPONGEZA UTENDAJI WA JPM, WATOA USHAURI MZITO.

 Mratibu wa Vijana wa Jamii Mpya ya Rais Magufuli Ally Makwiro akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Vijana wa Jamii Mpya ya Magufuli wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutendaji bora katika kipindi cha miaka mitatu kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwa manufaa ya watanzania wote.

Vijana wa jamii Mpya ya Magufuli ambapo chimbuko lake ni Tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam, licha ya kutoa pongezi wametaka kufanyika kwa maboresho katika sekta ya elimu kwa kutengeneza maslai ya walimu ambao wanaonekana kuwa na kipato kidogo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Vijana wa Jamii Mpya ya Rais Magufuli, Ally Makwiro, amesema kuwa mwalimu ni mtu muhimu kutokana wamekuwa na majukumu mengi tofauti na watumishi wengine wa serikali.

Bw. Makwiro amesema kuwa mwalimu wamekuwa akifanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila posho ya maji, umeme pamoja na makazi huku akitegemea msharaha wake wa tarehe 30.

"Tofauti na kufundisha mwalimu ni mshauri nasaha, askari, mwanajeshi, daktari, nesi, mzazi" amesema Bw. Makwiro.

Bw. Makwiro amesema kuwa elimu ya Tanzania iangaliwe kwa macho mawili hasa elimu ya msingi kutokana imekuwa ikihujumiwa kwa kuonyeshwa majibu na kwenda elimu ya sekondari wakiwa hawana uelewa wa kutosha.

Amesema kuwa ni vizuri Rais ambaye ni mtetezi wa wanyonge akafanya jambo la kimaslai kwa kundi la walimu jambo ambalo litasaidia kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa sera ya elimu kuleta tija kwa Taifa.

Hata hivyo amezitaka Mamlaka katika kazi ya mtaa, kata , halmashauri waishi kwa falsafa, maono na imani aliyokuwa nayo Mhe. Rais katika utendaji kazi katika miaka mitatu.

No comments