Ads

ABDUL NONDO ASHINDA KESI







Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo leo Novemba 5 ,2018.

ABDUL NONDO ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA

Swali la Hakimu la msingi, ni Je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga?? Pili, mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga.

Tatu, hakuna ushahidi toka jamhuri kuwa mshatikiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi wa hisia.

Nne, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa kwa kila namna na hata kielelezo kilicholetwa na Jamhuri kinatia mashaka sana, kwa mkanganyiko huu makahama imejizuia kuyaamini maelezo yaliyoletwa mahakamani.

Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatikiwa alitekwa au hakutekwa, hilo ni jukumu la polisi.

Hivyo basi, mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru.

Mwisho kabisa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unawashukuru mawakili wake waliosimamia kesi ya Abdul Nondo tangu mwanzo, lakini kipekee zaidi tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika hukumu hiyo.

Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2018. 
Na: THRDC

No comments