WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA.
Na Mwandishi Wetu Manyoni Singida
Wazee
na wasiojiweza waishio katika Makao ya Wazee Sukamahela yaliyopo
Wilayani Manyoni Mkoani Singida wamelalamika kupata aina moja ya chakula
kwa muda mrefu.
Hayo
yamesemwa na baadhi ya Wazee hao walipokuwa wakitoa malalamiko yao kwa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Dkt. Faustine Ndugulile alipotembela kujionea Huduma zinazotokewa katika
Makazi ya Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela.
Wazee hao wamesema wamekuwa wakipata hasa aina moja ya mboga aina ya maharagwe kwa mlo wa mchana na usiku kwa siku zote za wiki.
Akijibu
changamoto hizo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali inahudumia
Wazee na Wasiojiweza katika Makao 17 nchini na inaendelea kutoa huduma
stahiki kwa Wazee hao.
Dkt.
Ndugulile amemuagiza Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira
Mushi kupeleka fedha kwa wakati katika Makao ya Wazee na Wasiojiweza
nchini ili kuondokana na changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.
Pia
Naibu Waziri Ndugulile pia amemuagiza Afisa Ustawi Mfawidhi wa Makao
ya Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela kuandaa ratiba ya chakula stahiki
kwa ajili ya wahudumiwa na kuibandika katika eneo la wazi.
"Niseme
kuwa fedha zipo za kuwahudumia Wazee na Wasiojiweza katika Makao ya
Wazee na Wasiojiweza nchini watendaji timizeni wajibu wenu katika
kuhudumia kundi hili" Alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Akisoma
taarifa ya Makao ya Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela Afisa Ustawi
Mfawidhi wa Makao hayo Bw. Mgoo Senge amesema Makao hayo yanakabiriwa
na uchakavu wa majengo pamoja na kukosa ulinzi kutokana na kutokuwa na
uzio katika eneo hilo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile yupo mkoani Singida kwa ziara ya siku mbili kukagua
shughuli za Sekta ya Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jami

Post a Comment