WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA .
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Wavuvi ,wafanyabiashara na Mama Lishe wa Soko la Feri wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mke wake Mama Janeth Magufuli kwa mchango wao waliowapatia kwaajili ya kujenga ofis na kuendeleza biashara zao.
Mtakumbuka Rais alikuja mwaka 9 December 2015 baada ya kuapishwa alifanya usafi katika zone hiyo hiyo na wadau wetu walimlilia kilio na juzi alitoa hizo pesa kwa vikundi vyetu vya (UWAWAKI) na Mkewe naye alitoa kwaajili ya mamalishe tunamshukuru sana kwa mchango huo na upendo aliotuonesha , na kusimamia mabadilko katika soke hili ambalo ni lakimataifa na tunapigania kilasiku liwe na hadhi yakimataifa” alisema
Kwaupande wake mwenyekiti wa zone namba tatu ,Omary Mwinyi makungu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya wadau ,amesema kupatikana kwa fedha hizo kutasaidia kwani wamehangaika muda mrefu na wanamshukuru kwa kutambua mchango wao na kusema kuwa wao ndiyo walipambana hadi kuongezeka kwa mapato ya soko hilo kwa kupiga vita watu waliokuwa wakijinufaisha wao waowenyewe ambapo zamani makusanyo yalikuwa shilingi million 18 na sasa million 100.
‘’Hilisoko baada ya kupambana tuka pata bodi tumeanza kuyaona mafanikio na tuna mshukuru waziri Jafo , soko halikuwa hata na Akaunti akaagiza ikafunguliwa na sasa hataukarabati wa soko na ujenzi wa miundo mbinu inafanyika ‘’ alisema .
Amesema soko
la Feri ni moja ya masoko machache mazuri barani Afrika nila pili kwa ukubwa ukitoka
lilie la Senegal lakini wenzetu
wanaendesha vizuri soko lao na mapato yake yanazunguka hapo hapo lakini sisi
haikuwa hivyo baada ya sisi kupigania tuka itwa wezi ,ila nashukuru wametuelewa
sasa wezi na wadokozi hawapo tena .
Aidha
ameomba kupatiwa mafunzo kwa kikundi cha
ulinzi shirikishi maana kimetumika muda mrefu na kimesaidia sana na kusema kuwa
pamoja na kwamba kuna ulinzi kutoka SUMA JKT
lakini wasi sahaulike.
Naye Ashura Seif Nanjonga ,wa kikundi cha Baba na
Mamalishe UBAMALE akizungumza kwa niaba ya Mama na Baba lishe waliopewa
shilingi million tano amemshukuru Mama Janeth Magufuli na mumewe
kwa moyo wao walio unesha kwa kuwapenda wanyonge .
“ Pesa hizo
tumeziweka Bank wakati zinakuja kiongozi waetu hakuwepo ila sasa asharudi na
pesa hiyo tutaanza kuitumia kama tulivyo kuwa tumepanga hapo awali , katika
kikundi chetu tuko watu 50 na hatuna hata mabanda tuko juani hizi pesa zitatusaidia
angalau hata kwa kuweka kivuli hata
miamvuli ya kujikinga na jua na mvua’’alisema





Post a Comment