MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14
Hussein Ndubikile
Mwambawahabari
Kampuni
ya Miranda Sport imeandaa tamasha la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na wadau
wengine kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki
miaka 19 iliyopita.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tamasha hilo Kulwa Karedia, alisema tamasha hilo litapambwa na mashindano
ya riadha, mpira wa miguu,mashindano ya baiskeli na mkesha wakuabudu usiku wakuamkia Oktoba 14.
Amesema
kuwa tamasha hilo limepewa jina la Tamasha la Mwalimu Nyerere litashirikisha
wananchi kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara ikiwemo Tarime,Bunda,Musoma,Butiama
na Serengeti pamoja na mikoa jirani.
Karedia
amebainisha kuwa mbio zote zitaanzia Uwanja wa Mwenge wa Butiama kupitia Ofisi za halmashauri ya wilaya ya Butiama
kuelekea barabara ya Kiabakari ambao Mwalimu Nyerere aliutumia wakati wakuunga
mkono matembezi ya Azimio la Arusha mwaka 1967.
Amesisitiza
kuwa mbio zitahusisha urefu wa kilometa 10 kwa watu wa umri wa miaka 15
nakuendelea, kilometa tano kwa vijana wa miaka 13-18, na mbio za kilometa 12.5
Karedia
amesema kutakuwa na mashindano ya mbio za baiskeli zitakazo aanzia Butiama kupitia
Buswege-Buturugi,Sabasaba, Kiabakari hadi Butiama.
Ameongeza
kuwa kutakuwa na tamasha la mpira wa miguu ambapo timu tatu ambazo ni kombaini
ya Butiama, Kombaini ya Wilaya ya Serengeti na mabingwa wa kombe la Siro kutoka
kijiji cha kiabakari zitashiriki.
“Tumeamua
kumuenzi Mwalimu kupitia sanaa za michezo kwakuwa naye alikuwa mdau wa michezo,
pia tutakuwa na mkesha wakusifu nakuabudu ambapo vikundi vya kwaya vitakesha
vikisifu nakuabudu usiku wakuamkia Oktoba 14,” amesema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Utamaduni wa Wazanaki, Mashaka
Mgeta amewataka wakazi wa Butiama na mikoa ya jirani wajitokeze kwa wingi
katika maadhimisho ya kumbukidhi hiyo.
Zawadi
mbalimbali zitatolewa kwa washiriki na washindi katika mashindano hayo zikiwemo
seti za jezi, medali za shaba, baiskeli mpya na mipira na kiasi cha pesa
ambacho kitatangazwa baadae.
Mgeni
rasmi wa tamasha hilo anatarajiwa kuwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania
Pius Msekwa, na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa
mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ni miongoni mwa wageni waalikwa.
Kauli
mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo inasema Twende Butiama tumuenzi Mwalimu
Nyerere kwa vitendo.
Post a Comment