Ads

Wenye viwanda watakiwa kujiunga na CTI, Surbash Patel mwenyekiti mpya.



Na Hussein Ndubikile 
Mwambawahabari
Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) limewataka wanachama wake kuwa waaminifu na waadilifu ili kulinda heshima ya chombo hicho pamoja na kuifikisha nchi katika uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es  na Aliyekuwa Mwenyekiti wa CTI Dkt. Samuel Nyantahe wakati wa makabidhiano ya ofisi na Mwenyekiti mpya wa shirikisho hilo,Surbash Patel yaliyofanyika katika ofisi za CTI jijini humo.

“Tunakaribisha wenye viwanda kujiunga na na CTI kutokana na ukweli kwamba tuna viwanda vingi lakini wanachama ni wachache, pia tunasisitiza nidhamu, uadilifu na uaminifu kwa wanachama,”amesema.

Nyatahe amesema shirikisho hilo lina jumla ya viwanda 1600 lakini kuna wanachama zaidi 400 huku akiwawataka wenye viwanda ambao hawajiunga kujiunga na shirikisho ili kulifanya  liwe imara zaidi.

Dkt. Nyantahe amemkumbusha mwenyekiti mpya kuendelea  kushughulikia changamoto zinazolikabili shirikisho hilo ikiwemo Sera ya mambo ya kodi ambayo hubadilika badilika, ucheleweshaji wa kurejeshewa Kodi ya Ongezeko la Mapato (VAT), kuchelewa kutoa vibali vya kazi, kupandisha kwa ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazotoka nje pamoja na uwepo wa nishati ya umeme ya uhakika.

“Sauti ya viwanda itakuwa kubwa tutakapokuwa na wanachama wengi kwakuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu,”amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya Surbash Patel amemshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake na kuahidi kufuata nyayo zake na kuendelea kumtumia mtangulizi wake katika masuala yanayohitaji ufafanuzi zaidi.

“Nitashirikiana na wafanyakazi wenzangu pamoja na wanachama,kupaza sauti katika kushughulikia changamoto zinazohusu viwanda nchini,”amesema.

Surbash amebainisha kuwa atahakikisha CTI inafanya kazi kwa karibu zaidi na Serikali ya Awamu ya Tano ili kufanikisha adhima uchumi wa kati kupitia sekta hiyo ifikapo mwaka 2020.

Ameongeza kuwa katika uongozi wake atawasaidia wanachama kutatua changamoto zao lakini hatakuwa tayari kuwasaidia wanachama watakao kwenda kinyume na sheria zinazoongoza CTI.

Naye Makamu Mwenyekiti wapili wa CTI, Shabbiri Zavery alitoa wito kwa watanzania kuthamini,kupenda na kununua bidhaa za ndani ili kujenga uchumi wa Tanzania.

“Ninawahimiza watanzania waone fahari ya kutumia bidhaa zinazo zalishwa nchini kwakufanya hivyo viwanda vyetu vitakua na mtaji wakuzalisha bidhaa bora,”amesema.

No comments