Ads

THPS, WIZARA YA AFYA YAWAJENGA UWEZO WATUMISHI WA AFYA KUTUMIA NJIA YA MTANDAO Tele-ECHO.


Mkurugenzi Uhakiki wa Huduma Bora za Afya Dkt Mohammed Ali Mohammed akiwa Na wadau kutoka taasisi mbalimbali katika sekta ya afya  leo jijini Dar es Salaam katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa Afya.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya THPS (Tanzania Health Promotion Support) kwa kushirikiana Wizara ya Afya Maendelea ya Jamii  Jinsia, Wazee na Watoto  inaendelea kutoa mafunzo ya uendeshaji kwa njia ya mtandao (Tele-ECHO) kwa wataalam wa afya  ili kuwajengea uwezo wa upimaji wa ugonjwa wa ukimwi.

Mfumo wa program ya ECHO inatumia mtandao kutoa elimu jambo ambalo inasaidia kuwafika watu wengi pamoja na kupunguza gharama za usafiri kwa washiriki kutoka sehemu moja kwenda nyengine kwa ajili ya kushirikia mafunzo hayo.

Akizungumza leo jiini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa njia ya mtandao, Mkurugenzi Uhakiki wa Huduma Bora za Afya Dkt Mohammed Ali Mohammed, amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia sana kuwafikia wataalamu wengi kwa muda mfupi.
Mkurugenzi Uhakiki wa Huduma Bora za Afya Dkt Mohammed Ali Mohammed akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

Dkt Mohamed amesema mfumo kwa njia ya mtandao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya hasa maeneo ya vijijini.

Amesema mfumo huo utaweza kuwafikia watoa huduma kwa asilimia kubwa sambamba na kupunguza gharama za mikutano.

"Rais Dkt. John Magufuli alipozindua mtandao wa TTCL alisisitiza tuanze kutumia mafunzo kwa kupitia masafa ili kupunguza gharama za safari na kuhakikisha tunawafikia watu wengi kwa wakati mmoja ” amesema Dkt Mohamed.

 Dkt Mohamed ambaye alikuwa anamwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali, amesema kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau ina mikakati ya kufunga vifaa maalumu vya mfumo huo katika vituo vya afya vilivyopo katika hospitali za rufaa za mikoa ikiwemo Dodoma, Kagera, Pwani, Arusha, Tanga ambavyo  vitaunganishwa katika Hospitali  ya Taifa Muhimbili.

Dkt. Mohamed amefafanua kuwa  kwa mujibu wa sheria ya maabara namba 22 ya mwaka 2007 inawataka watu wote wanaofanya vipimo vya maabara wapatiwe leseni (certification).
 Mkurugenzi wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya THPS (Tanzania Health Promotion Support) Dkt. Rebeka Mbatia akifanya mahojiano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya THPS (Tanzania Health Promotion Support) Dkt. Rebeka Mbatia, amesema kuwa mfumo wa program ya ECHO ni mzuri kutokana inatumia njia ya  mtando kutoa elimu na kuwafikia watu wengi.

Dkt. Mbatia amesema kuwa lengo la programu ni kuhakikisha watumishi wa Afya wanaofanya vipimo vya ugonjwa ugonjwa wa Ukimwi wanatoa majibu sahihi.

"Kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watumishi wa Afya wamekuwa wakitoa majibu sio sahihi katika upimaji wa VVU"amesema Dkt. Mbatia.

Amefafanua kuwa mradi huo ni wa muda wa miaka mitando ambao umelenga kuwajenga uwezo watumishi wa Afya katika kupima ugonjwa wa Ukimwi.

Amesema katika Mwaka wa kwanza wa utekelezaji wapimaji I,000 watapata mafunzo hayo ambayo yatakuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya Afya.
"Mfumo huu ni mzuri kwani baada ya muda mfupi utasaidia kuongeza watendaji wa Afya katika upande wa maabara" amesema Dkt. Mbatia.

Mkurugenzi wa Mafunzo Dkt. Donard Mbando amesema vituo vya afya vilivyoanza kutekeleza mpango huo wa kupata mafunzo hayo  ni pamoja na mkoa wa Shinyanga, Iringa, Njombe na Mbeya.

Dkt. Mbando ameishukuru wizara ya afya kwa mchango wao katika kufanikisha utekelezaji wa utoaji wa mafunzo kwa njia ya mtandao.

Mafunzo kwa njia ya mtandao yamewashirikisha wadau mbalimbali  Wizara ya Afya Maabara ya Taifa kutoka mikoani Dodoma, Morogoro pamoja na Hospitali ya Kibong’oto ya kifua kikuu.

Lengo la mafunzo hayo ni uhakikisha wataalamu wa maabara wanafanya kazi yao kwa uweledi hasa katika kuwapa majibu sahihi watu wanapopima virusi vya ukimwi.

Mfumo wa utoaji mafunzo kwa njia ya mtandao TeleECHO ulianza mwaka 2016 kwa kuanza kutumia katika hospitali nne za mikoa ambazo ni  Mbeya, Iringa, Njombe pamoja na Shinyanga.

No comments