MSIMAMIZI WA UCHAGUZI ILALA AVIONYA VYAMA VYA SIASA KUTOTUMIA VIONGOZI WA DINI KATIKA KAMPENI.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri, akizungumza na waandshi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa
Manispaa ya ilala mapema leo ( Picha na John Luhende)
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Msimamizi wa
Uchaguzi wa Maispaa ya Ilala ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo Jumanne Shauri , amevitaka
vyama vyote vya siasa vinavyo shiriki uchaguzi wa Ubunge jimbo la Ukonga na udiwani katika kata za Zingiziwa na
Vingunguti kufuata sheria na maadili ya uchaguzi ili kuepuka vurugu zinazoweza
kujitokeza.
Msimazi huyo
ameyasema hayo leo wakati akizunguza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa
kampeni zinazoendelea wilayani Ilala nakusema kuwa kampeni zinaendelea
vizuri japo kuna malalamiko macheche
huku akivionya vyama vya siasa kutotumia viongozi wa Dini katika kampeni zao.
‘’kuna suala la kutumia viongozi wa dinini katika kampeni mimi
kama msimamizi wa uchaguzi nasema kama
kunachama chochote cha siasa kitakacho tumia viongozi wa dini tutakipa adhabu”amesema.
Aidha
ameviasa vyama hivyo kujikita zaidi katika kunadi Ilani za vyamavyao badala ya
kuzumnguza matusi na maneneo ya kibaguzi ili wananchi waweze kuchagua
wayoitaka.
Pamoja
nahayo Msimamizi huyo ameeleza namna
uchaguzi huo utakavyo endeshwa siku ya kupiga kura,kwamba vituo vya kupigia
kura vitafunguliwa saa moja asubuhi hadi
saakumi jioni na kufuatiwa na zoezi la kuhesabu kura.

Post a Comment