Ads

Baraza la Mazingira latoa wito kwa Kampuni na mashirika




Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Upanga Mashariki Rukia Rihami akisubiri kupewa tuzo ya usafi kutoka kwa Msajili wa Baraza la Afya Idd Hoyange Dar  es Saalam leo  katika madhimisho ya siku ya Afya ya Mazingira Duniani yalioandaliwa na Manispaa ya Ilala,


Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
BARAZA la Afya Mazingira latoa wito kwa Kampuni Binafsi kujitokeza kuwekeza katika  huduma za afya ya mazingira ili kusaidia Halmashauri kudhibiti maambukizi ya magojwa mbalimbali katika jamii.

Wito huo umetolewa Dar es salaam jana na Msajili wa Baraza la Afya na  Mazingira Idd Hoyange wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya ya mazingira Duniani ambapo alimwakilisha Mkuu wa wilaya Ilala Sophia Mjema.

Idd alisema kuwekeza katika elimu ya udhibiti  wa magojwa kwa kuimalisha afya ya mazingira ni muhimu kwani tutafanikiwa kuzuiya magonjwa ambayo mengi yanazuilika kwa urahisi na  hivyo kupunguza gharama kubwa za matibabu ya magojwa hayo.

"Baraza la mazingira latoa wito kwa kampuni na mashirika
hii itatoa fursa kwa jamii kushiriki katika kazi za ujenzi wa Taifa bila kusumbuliwa na maradhi hasa katika   hiki ambacho Taifa  linahitaji kufika katika uchumi wa viwanda"alisema Idd.

Idd alisema Shirika la Afya Duniani katika utafiti zilizofanyika duniani zinaonyesha watu takribani milioni 600 upatwa na magojwa yatokanayo na ulaji wa vyakula visivyo salama ambapo asilimia 40 ni watoto walio chini ya miaka mitano.


Aidha alisema watu 420,000 hufariki dunia na kati ya vifo hivyo 125,000 ni vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano (WHO.2015 .

Pia shirika linaeleza kuwa kama hatua madhubuti za kinga ya magojwa,uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka.

No comments