ZIARA YA DC MJEMA YAMUIBUAMTUHUMIWA WA MBAKAJI SUGU PUGU.
Mwamba wa habari
Na John Luhende
Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Mhe Sophia Mjema ameamuru kukamatwa na kuwekwa ndani pamoja na kufanyiwa uchunguzi kwa mkazi mmoja
wa Pugu mnadani mara baada yakulalamikiwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakimtuhumu kumbaka mtoto wake wakike
anayekadiriwa kuwa na miaka saba.
Shutuma hizo
zimetolewa na wakazi hao katika mkutano wa DC
Mjema ulifanyika Pugu mnadani kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi wa
eneo hilo ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake jimboni ukonga kusikiliza kero za
wananchi na kuzipatia majawabu.
Mkazi mmoja huyo ambaye jina lake tumelihifadhi anaeleza namna mtoto huyo anavyoishi mazingira magumu kwa sababu ya vitendo vya kikatili anavyo katendewa na Babayake.
Mkazi mmoja huyo ambaye jina lake tumelihifadhi anaeleza namna mtoto huyo anavyoishi mazingira magumu kwa sababu ya vitendo vya kikatili anavyo katendewa na Babayake.
Msamalia
mwema huyo ameendelea kudai kuwa hata majirani wanafahamu kuhusu jambo hilo lakini wamekuwa wakikosa ushirikiano kutoka
kwa baba huyo kujua ukweli kuhusu maisha ya mtoto huyo.
Mara baada ya
madai hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia
Mjema , alimwita mtuhumiwa huyo lakini alikuwa ameshanza
kutoroka mkutanoni hapo na kwenda
kubadili mavazi aliyokuwa nayo mwanzo lakini akafuatwa na kukamatwa huku akijitia mwenda wazimu akijibu mambo
tofauti na anacho ulizwa.
Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani pindi
uchunguzi wa kipimo cha DNA utakapo fanyika kama
alivyo agiza DC Mjema , na mtoto huyo kwa sasa yuko amepelekwa hospitali hapa jijini Dar es Salaam.
Post a Comment