BARAZA LA MADIWANI ILALA WAMSIMAMISHA KAZI MKANDARASI.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akiongoza kikao cha baraza la madiwani


Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam leo kimeadhimia kuisimamisha kampuni ya usafi ya Seizeri East Afrika Limited kwa madai ya kutofata sheria na taratibu.
Akizungumza katika kikao cha robo ya nne cha baraza la madiwani Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amesema kampuni hiyo ilipaswa kuelimisha wananchi na sio kuwatoza faini kiholela.
Kuyeko amesema wamewapatia semina ya namna wanatakiwa kuepuka kuwapiga wananchi faini kilolela jambo ambalo limekuwa kero kwa jamii.
Diwani wa kata ya Segerea Edwin Mwakatobe ambaye aliuliza kwenye kikao hicho kuhusiana na ufanyaji wa kazi wa kampuni hiyo,amesema kwenye kata kuna watendaji wa ufanyaji wa usafi iweje kampuni hiyo ikamate watu na kuwapiga faini.
Katika hatua nyingine moja ya mjadala ambao umejadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na suala la kuchinja ambapo wachinjaji wametakiwa kufata sheria na taratibu za uchinjaji ili kuweza kuepukana na changamoto zinazojitokeza.
Hata hivyo kwa pamoja Wajumbe wa baraza hilo likiongoza na wmenyekiti wa baraza Meya wa Ilala Kuyeko pamoja na Katibu wake Kaimu Mkurugenzi wamemuaga Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya IlalaMsongela Palela ambaye amefanyiwa mabadiliko kikazi na Rais Magufuli na kuhamishiwa Halmashauri mpya ya wilaya ya Kalambo
Post a Comment