YANGA WAAHIDI MAKUBWA TAIFA LEO.
Kikosi cha Yanga kinashuka dimbani kucheza na Mtibwa Sugar leo ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili kwa msimu wa wa 2018/19.
Kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, ameahidi kuwa Yanga itauwasha moto mkali.
Nyika amepata jeuri hiyo baada ya kuwamaliza USM Alger kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Agosti 19 ambapo waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mwenyekiti huyo anaamini Yanga itaonesha maajabu zaidi ya yale waliyompatia Alger kwa kuwa wana malengo ya kurejesha kikombe chao ambacho kilikwenda kwa wekundu wa Msimbazi, Simba.
Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 12 za jioni ambapo pia itakuwa mubashara kupitia king'amuzi cha Azam TV.
Post a Comment