WAISLAMU LEO KUSHEREKEA IDD EL HAJJ
WAISLAMU nchini leo wanaungana na Waislamu wenzao katika nchi mbalimbali, kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj. Katika taarifa yake iliyotolewa hivi karibuni, Kaimu Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma, alihimiza Waislamu wote kusherehekea siku hiyo kwa amani.
Akimnukuu Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir, Katibu mkuu huyo alisema maadhimisho ya sikukuu hiyo kitaifa yatafanyika jijini Dar es Salaam. Pia alisema swala ya Idd leo hii itafanyika katika Uwanja wa Msikste Tamaa uliopo Vingunguti na Baraza la Idd litafanyika hapo hapo baada ya swala hiyo.
Post a Comment