Ads

SHIRIKA LA THAMINI UHAI YAOKOA VIFO VYA WATOTO, WAKINAMAMA KIGOMA.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali Thamini Uhai, Dkt. Nguke Mwakatundu akifafanua jambo leo Jijini Dar es Salaam wakati akielezea tathmini ya utafiti utendaji wa shirika hilo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza jambo mbele ya wadau mbalimbali wa afya leo Jiji Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Shirika lisilo la Kiserikali la Thamini Uhai limefanikiwa kupunguza idadi ya vifo vya watoto na wakinamama wajawazito baada kuvijengea uwezo vituoa vya afya 46 mkoani Kigoma.

Thamini Uhai imefanikiwa kutoa elimu ya  utoaji huduma bora, salama, dharura na uzazi katika vitoa vya afya mkoani Kigoma na kupunguza idadi ya vifo.

Takwimu za mwaka jana zimeonyesha jumla ya uzazi 28,23I zimefanyika katika vituo 33 katika mradi Thamini Uhai mkoani Kigoma ambapo ni ongezeko la I0% ikilinganisha na mwaka 20I7 na kupunguza idadi ya vifo wakati wa kujifungua.

Akizungumza katika hafla ya utafiti wa tathmini, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Thamini Uhai, Dkt. Nguke Mwakatundu, amesema kuwa katika utendaji wao wamefanikiwa kutoa msaada wa kuvijengea uwezo vituo vya Afya.

Amesema kuwa baada ya kuvijengea uwezo vituo vya afya imesaidia kwa kiasi kikubwa, kwani jumla ya upasuaji 2,509 umefanyika mkoani kigoma  mwaka jana  ambapo ni ongezeko la asilimia I5 ukilinganisha na mwaka 20I6.

Dkt. Mwakatundu amesema kuwa mradi unaendelea kuwajengea uwezo wahudumu katika uokoaji wa watoto wachanga kupitia mradi maalum wa 'Kangaroo Mather Care and Helping Babies Breathe.

"Msaada huu utasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga waliozaliwa na matatizo ya kupumua kwa 79%" amesema Dk. Mwakatundu.

Amefafanua kuwa kupitia mradi huo jumla ya watoto wachanga I,433 waliokolewa maisha yao kwa mwaka jana.

Ameeleza kuwa kuna mpango mwengine  mama msindikizaji unaoendeshwa katika vituo vya afya mkoani Kigoma ambao umelenga kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama.

"Tunaendelea kubadilishana uzoefu kuhusu mpango wa Thamini Uhai kama mfano wa kuigwa ambao utasaidia kufikia malengo yaliyowekwa katika mpango wa Afya ya uzazi wa one plan II ya kupunguza vifo vya uzazi kutoka 556 hadi 292 kwa kila vizazi hai I00,000" amesema Dk. Mwakatundu.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema kuwa ni jitihada nzuri ambazo zimefanya na Thamini Uhai kwa ajili ya kuokoa vifo vya watoto  na wakinamama.

Mhe. Ummy amesema kuwa upo uwezekano wa kuokoa vifo vya watoto wachanga na wakinamama wakati wa kujifungua kama kila mganga mkuu wa mkoa hatafanya maboresho katika utendaji wao.

Amesema kuwa waganga wakuu wanapaswa kuchua hatua ili kuhakikisha huduma zote katika vituo vya afya zinatolewa katika mazingira rafiki.

"Natoa maagizo hospitali zote za rufaa zinatakiwa kuwa na mipango mahususi wa kupanga ratiba za kutembelea vituo vya afya kila baada ya miezi mitatu pamoja na kuwajengea uwezo watoa huduma" Mhe. Mwalimu.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Mganga, amesema kuwa baada ya taarifa ya utafiti kutoka Thamini Uhai sasa tumebaini kujifungua sio kifo.

Amesema kuwa thamini uhai wameonyesha ushirikiano mkubwa kwa serikali katika kuhakikisha wanapungua vifo vya wakinamama.

Mganga amesema kuwa wameonyesha juhudi kubwa ambazo zimeleta matokeo chanya kwa taifa.

"Thamini Uhai wametoa mchango mkubwa katika sekta ya afya kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo vyombo vya kusafirisha wagonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyengine" amesema Emmanuel.

No comments