Ads

MKURUGENZI SHULE ZA AL MUNTAZIR ISLAMIC AFUNGA MASHINDANO YA DEBATE, AWAPONGEZA WASHIRIKI


Mkurugenzi wa Shule za Seminari  Al -Muntazir Islamic Mahmood Ladak, akimpongeza mwanafunzi wa shule hiyo baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya mdahalo yaliomalizika leo jijini Dar es Salaam.
Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shule za Seminari Al Muntazir Islamic (Al Muntazir Islamic Seminary) amezitaka shule mbalimbali hapa nchini kuwa na utamaduni wa kushiriki katika mdahalo jambo ambalo litasaidia kuongeza ufanisi kwa wanafunzi katika masomo yao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mdahalo wa (Mwalimu Nyerere School Inventation debate championship) Mkurugenzi wa Shule zote za Al -Muntazir Islamic Mahmood Ladak,  amesema kuwa ushiriki wa wanafunzi katika mdahalo unamuwezesha kujiamini na pamoja na kufanya vizuri katika mambo mbalimbali.

Ladak amesema kuwa mashindano hayo yamefanyika kwa muda siku tatu katika shule ya Seminari ya Al Muntazir Islamic na kuwakutanisha wanafunzi wa sekondari barani afrika ambapo imewasaidia sana wanafunzi kuongeza uwezo wa kujieleza na kujiamini katika kuongea na kupanga hoja zao.

Mkurugenzi huyo ameeleza  kuwa lengo la mashindano ni kuwakutanisha wanafunzi wa kitanzania na wezao kutoka kutoka nchi mbalimbali ili kubadilishana mawazo ya kielimu waliojifunza darasani kupitia madahalo.

"Nawapongeza wanafunzi wote walioshiriki kwani wamefanya vizuri na wote ni washindi" amesema Ladak.

Hata hivyo ameishukuru Tanzania Competitive Phetoric Organization (TCRO) kwa kufanya maandalizi ya mdahalo huo ambao umekuwa chachu ya maendeleo kwa wanafunzi walioshiriki.



Naye mwanafunzi wa shule ya Al Muntazir Islamic Rahmat Rashid, amesema kuwa mashindano yalikuwa  maziri kutokana na ushindani uliokuwepo.


Rashid ambaye anasoma kidato cha sita ameeleza kuwa kujiamini kwake wakati wa kuchangia mada mbalimbali kumemfanya afanye vizuri katika kipengele cha kuzungumza.


Naye mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Shaaban Robert Eben Mnzava, amesema kuwa jitihada zao pamoja na kumuomba mungu ni miongoni mwa sababu zilizowafanya kushika nafasi ya kwanza katika mdahalo huo.


"Ni jitihada zetu zimetufanya kushika nafasi ya kwanza katika mashindano haya pamoja na kuwa karibu na mungu kwa maombi" amesema Mnzava.


Kwa upande wake Mratibu wa mashindano ya Mwalimu Nyerere school Inventation debate championship  kutoka  TCRO Batulaine Immaculate, amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yamekwenda vizuri.


Amesema kuwa kila shule imeshiriki vyema katika mdahalo jambo ambalo limeongesha ushindani mkubwa katika kuhakikisha kila shule inafanya vizuri.


"Ushindani ulikuwa mkubwa sana kati ya shule za Tanzania na nje ya nchi... tumeona shule ya Shaaban Robert imefanikiwa kuwa mshindi wa kwanza baada ya kuingia fainali na shule ya Zimbabwe"amesema Immaculate.

Immaculate amebainisha kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano ya mdahalo kwa mwaka huu, sasa wanajipanga katika mashindano yajayo ili zishiriki shule nyingi.

Mashindano ya mdahalo kwa mwaka huu yamekutanisha wanafunzi zaidi ya 200 kutoka shule mbalimbali barani afrika.
Miongoni mwa nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Zimbabwe, Zambia na Namibia.
Baadhi ya shule zilizoshiriki hapa nchini ni pamoja na  Al Muntazir Islamic Seminary, Shaaban Robert, Feza Boys, Feza Girls, Agha khan pamoja na Tusiime.
Mwanafunzi wa Shule ya Al Muntazir Islamic Rahmat Rashid akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya vizuri katika mdahalo.
Mwanafunzi wa Shule ya Shaabn Robert Eben Mnzava akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya shule yake kushika nafasi ya kwanza katika mdahalo wa Mwalimu Nyerere Schools Inventation  Championship.


Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Cateway ya Zimbabwe Dadiso Chitengwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya shule yake kufanya vizuri na kushika nafasi ya pili.

No comments