MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO.
Na. John Luhende
Mwamba wa habari
Mbunge wa
kuteuliwa Mama Janeth Masaburi amehitimisha ziara yake ya sikutatu yakutembela
mkoa wa Dar es salaam kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi .
Mbunge
Masaburi amehitimisha ziara hiyo kwa kuzungumza na wanachama na wenyeviti na wajumbe
wa nyumba kumi wa CCM Kitunda na Kivule ,ambapo amewataka viongozi na wanachama
kushikamana kwa pamoja ilikuhakikisha Ukonga wanaikomboa kuoka upinzani katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na na
jimbo lote la ukonga lina kuwa chini ya
CCM.
“Lazima
tubaini kero zote zilizopo katika mitaa yetu mapema na kuzitatua
ili tusije kutumia jasho jingi
Damu kidogo wakati wa vita tutatoa jasho kidogo na hatuta hema sana wakati wa
uchaguzi wa serikali za mitaa” alisema .
Aidha
amewataka kuacha ubinafsi na nongwa
ilikupata viongozi wanafanyakazi kwaajili ya kuwaletea maendeleo wananchi na kuwataka
kuelewa kuwa serika msingi wake ni serikali za mitaa ili kupata viongozi bora kunahitaji mshikamano.
“Upinzani
tuliuruhusuwenyewe kwa sababu ya ubinafi mmeona wenyewe mlipata kunyapaliwa mkitaka huduma mlinyimwa hadi vyandarua
mlinyimwa , kunasiku utataka huduma au
ndugu yako atataka huduma atazikosa kwa kwasababu wewe ulitumia wivu tu kwa
kumkomoa mtu kwa makosa madogomadogo acheni wivu.” Alisema.
Hatahivyo Masaburi, amewataka wajumbe hao kuwanyenyekea
wanachama na wananchi kwakuwa wao wakopale kwaajili yakuwatumikia.
Katika ziara
hiyo Janeth Masaburi ameatembelea maeneo
yahuduma za kijamii ikiwemo kituo cha
afya Buguruni mnyamani , pamoja
na kupongeza huduma nzuri zinazotolewa ,ameutaka uongozi wa kituo hicho pamoja
kuweka mikakati madhubuti ilikuboreshahuduma
ikiwemo upanuzi wa eneo na kufikiria kujenga Majengo ya ghorofa, pia akawataka
wakala wa baraba za mjini na Vijijini TARURA kuongeza kasi ya ujenzi wa
barabara ya Buguruni kwa myamani ili kuondoa usumbufu wanao upata wanachi
hasa wanao enda kutibiwa katika Kituo cha Afya Buguruni kwa Mnyamani .
Maeneo
mengine aliyo tembelea ni pamokoja na mradi
wa visima virefu vya maji Wilaya Kigamboni ambao unatekelezwa na Mamlaka ya
Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam (DAWASA)
Mhe. Masaburi amesema kuwa ni vyema serikali
ikaongeza nguvu katika kukamilisha mradi huo wa maji ambao utakuwa msaada
katika kuondoa na kero ya ukosefu wa maji.
"Mradi huu ukikamilika wakazi wa Dar es Salaam
itakuwa historia kuhusu ukosefu wa maji" amesema Mhe. Masaburi.
Amesema kuwa visima hivyo vina maji ya
kutosha, hivyo wananchi wanapaswa kutunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha
vinawasaidia.
Mhe. Masaburi amesema kuwa serikali inaendelea
kutekeleza miradi mbalimbali ili kuhakikisha inatatua changamoto ambazo
zimekuwa kikwazo katika maendeleo.
"Naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa
jitahada zake katika kuhakikisha inatekeleza miradi ya kimaendeleo"
Ukitaka kuifahamu CCM nenda site" amesema Masaburi na kuongeza.



Post a Comment