MBUNGE JANETH MASABURI AHIMIZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA WA DSM.
Mwambawahabari
Mbunge wa kuteuliwa na Rais Mhe Janeth Masaburi amewataka wakala wa baraba za mjini na Vijijini TARURA kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Buguruni kwa myamani ili kuondoa usumbufu wanao upata wanachi hasa wanao enda kutibiwa katika Kituo cha Afya Buguruni kwa Mnyamani .
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Masaburi pia amekagua barabara ya barakuda eneo la highland baakuelekea Vingunguti na barabara yakitunda Kivule, Daraja la Kivule na ujenzi wa Daraja la kerezange na pamoja na maeneo mbalimbali katika wilaya Ilala na kuzitaka Mamlaka zinazohusika kuchukua hatua.
Mbunge Masaburi, ameanza ziara ya Mkoa mzima kwaajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, akiwa katika kituocha afya Buguruni Mnyamani pamoja na kupongeza huduma nzuri inayotolewa ameutaka uongozi wa kituo hicho pamoja kuweka mikakati mathubuti kulikuboreshahuduma ikiwemo upanuzi wa eneo na kufikiria kujenga Majengo ya ghorofa.




Post a Comment