ZIJUE FAIDA ZA KUJIUNGA NA BIASHARA CLUB YA KCB BENKI
Biashara Club
ni mfumo uliyoundwa mahususi kwa ajili ya kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara
wanaotumia huduma za kibenki kutoka benki ya KCB kuweza kufahamiana na
kubadilishana uzoefu katika mambo ya kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Benki Bw. Cosmas Kimario akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo jijini Dar es salaam katika mkutano na wadau wa Benki hiyo.
Akiongea na waandishi
wa habari mapema leo jijini Dar es salaam baada ya mkutano kati ya benki hiyo
na wateja wake Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Benki Bw. Cosmas Kimario alisema kuwa
club hiyo inafaida kubwa kwa wafanyabiashara kwa kuwa inawakutanisha wafanya
biashara wengi wa ndani na nje ya nchi kuweza kukaa pamoja na kujadili mambo ya
kibiashara, changamoto na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi.
Katika mkutano
huo uliofanyika mapema leo julai 25 katika hoteli ya Serena uliwakutanisha
zaidi ya wafanyabiashara 250 wa ndani na miongoni mwao wakiwa wafanyabiashara
wakubwa wa kati na wafanya biashara wadogo waliopo katika club hiyo ya KCB
Biashara.
Mkurugenzi huyo
aliongezea kuwa benki ya KCB inawapa fursa mbalimbali wafanyabiashara hao kwa
kuweza kutembelea nchi mbalimbali ili kuweza kujifunza mambo mengi zaidi kutoka
kwa wafanyabiashara wakubwa na kuweza kufanya biashara nao ili kupanua wigo wa
biashara zao, ikiwa kwa mwaka jana walitembelea nchi ya China na kwa mwaka huu
walipata nafasi ya kwenda nchini Japani.
“Lakini pia
ziara hizi zimekuwa na manufaa makubwa kwa wafanya biashara kuweza kukutana na
watu wanaofanya nao biashara kwa kutumia njia ya simu na mtandao lakini hapa
wataweza kuonana nao Mubashara na kujadili vitu vingi kuhusu biashara, ikiwa
kupata mapunguzo ya bei za bidhaa endapo wataagiza na pia wanatengeneza
uaminifu na wafanya biashara hao” alisema Mkurugenzi
Mshauri wa Masuala ya biashara Bw. Adolf Lymo akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya KCB.
Kwa upande wake Mshauri wa mambo ya kodi kwa wafanyabiashara Bw. Adolf
Lymo alisema kuwa kwa leo amekuja kutoa elimu ya ulipaji kodi na faida zake, kwa
wafanyabiashara wakubwa wadogo na hata wakati ili wajue kulipa kodi ndio msingi
wa maendeleo kwa taifa lolote duniani.
"Changamoto kubwa wanayokutana nayo wafanyabiashara wengi ni kupuuzia na
kutozingatia ulipaji wa kodi na kujisahau kuwa unapokuwa na biashara yeyote
basi ujue kuwa serikali nayo inakuwa ni mbia kwenye biashara hiyo kwa kutegemea
kuendesha vema maendeleo yake kupitia kodi yako".Alisema Adolf
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia mkutano kwa makini
Post a Comment