Ads

YANGA BADO IPO SANA



Na John Luhende
 Mwambawahabari 
Wanachama na mashabiki wa  Club ya Yanga wametakiwa kuwa na umoja kushangilia timu yao ambapo ina tarajiwa kucheza mechi na timu ya Gormahia ya Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa club Dimas Ten, amesema Yanga inatarajiwa kushuka dimbani  kukipiga  na timu ya Gormahia siku ya Jumapili na kuwakamata wazi kuwa kiingilio kitakuwa ni shilingi 7000 Vip na 3000 kwa kawaida.

Aidha amesema mchezaji timu ya Singida United Feisal Salum  Abdallah imekubali kumwachia mchezaji huyo iliachezee timu ya Yanga. 

Mapema mwezi huu Feisal , alizua sintofahamu baada ya kutambulishwa na klabu mbili katika siku moja, asubuhi Singida United na jioni Yanga, wote wakisema wamemsaini kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka JKU ya Zanzibar.


"Ziko taarifa nyingi kuhusu wachezaji wetu nataka niwaelezetukuwa siku chache tutatoa taarifa rasmi" Amesema
Baada ya kujiuzulu Sanga,  Kamati ya utendaji kwa kushirikiana na bodi ya wadhamini imemteua Omar Kaya kuwa Katibu mkuu atakaye simamia shughuli zote ikiwemo usajili
Akizungumzia kuhusu nafasi zilizo achwa wazi na viongozi waliojiuzulu Amesema kamati bado inashughulikia kuhusu kuziba nafasi  hizo.

No comments