LHRC YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA KWA MGOMBEA WA CCM HUKO TUNDUMA
Kituo
cha Sharia na Haki za Binadamu kimesikitishwa na kitendo cha wananchi
kujichukulia sharia mkononi kilichojitokeza katika kata ya Tunduma,
Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya Tunduma na kuelezwa kuwa kitendo hicho
uvunjaji wa sheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Anna Henga akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema jijini Dar es salaam Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo hicho Bi. Anna Henga alisema kuwa mgombea huyo
alichomewa moto nyumba yake baada ya kuhama kutoka Chama cha Demokrasia
na Maendeleo(CHADEMA) na kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM.
“Kituo
cha Sharia na Haki za Binadamu kinakemea vikali kitendo hicho kwani
kila mtu anahaki ya kuchagua, kuchaguliwa au kujiunga na chama chochote
bila kujari hisia za watu wengine, hivyo kitendo cha kutishia maisha
yake ni kukiuka haki za binadamu hususani haki kuu na ya msingi ya
kuishi” alisema Anna Henga
Aliongezea
kuwa kumekuwa na hali ya sintofahamu kwa wananchi katika kata zipatazo
30 ambapo wananchi wamepokonywa haki yao ya kuchagua viongozi katika
uchaguzi mdogo wa marudio, Na ikielezwa kuwa baadhi ya wagombea hususani
wa vyama vya upinzani wameenguliwa kutokana na sababu mbalimbali
zikiwemo tuhuma za kutokidhi vigezo vya kiufundi, na baadhi ya vigezo
hivyo vimeelezwa kuwa kutojua kusoma na kuandika pamoja na vigezo vya
kutokuwa raia wa Tanzania.
Wakati kwa mujibu wa ibara ya 13(4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 Imeeleza kuwa
“Ni
marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yeyote
inayotekekeleza madaraka yake nchini ya sharia yeyote au katika
utekelezaji wa kazi au shuguli yeyote ya mamlaka ya nchi” Mwisho wa kunukuu
Post a Comment